Shajara ya mwana-Mzizima no. 3 iko njiani inakuja

Shajara ya mwana-Mzizima no. 3 iko njiani inakuja

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
1565031806564.png


1565031842143.png


Shajara ya Mwana-Mzizima No. 3 iko njiani inakuja.

Cover ya kitabu hiki kwa hakika inavutia kwani inamwonyesha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameshika bango lisemalo, ''Uhuru Kamili 1961.''

Huyu mbele kulia pembeni ya Mwalimu Nyerere kwa mbele ni Sheikh Issa Nasir wa Bagamoyo na pembeni yake yuko Bi. Mugaya Nyang'ombe mama yake Baba wa Taifa na nyuma ya Bi. Mugaya katika yake na Sheikh Issa Nassir ni Oscar Kambona na upande wa kulia wa Mwalimu Nyerere yuko Rajab Diwani.

Hii picha ilipigwa Karimjee Hall Waziri wa Makoloni Ian Macleod alipokuja kutoa tarehe ya uhuru wa Tanganyika.

Sheikh Issa alikuwa siku zote akikaa karibu sana na Mwalimu Nyerere.

Angalia picha ya Baraza la Wazee wa TANU mwaka wa 1955 Sheikh Issa amechutama chini ya Mwalimu Nyerere ameegemeza fimbo kwenye bega lake la kushoto.
 
Back
Top Bottom