Shajara za vita za lance corp0ral Kleist Sykes vita vya kwanza vya dunia (1914- 1918)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SHAJARA ZA VITA ZA LANCE CORPORAL KLEIST SYKES
(1894 - 1949)

VITA VYA KWANZA VYA DUNIA 1914- 1918

Utangulizi

November 11, 1918 ndiyo siku Vita Vya Kwanza Vya Dunia vilimazilizika na dunia inaadhimisha siku hii.

Kleist Sykes hajaacha kunishangaza kila ninapoyaangalia maisha yake kupitia mswada alioandika kabla hajafa mwaka wa 1949 mswada ambao alimwachia mwanae Abdul Sykes na yeye Abdul akampa binti yake Aisha Daisy Sykes na Daisy akiwa mwanafunzi wa Historia Chuo Kikuu Cha Afrika Mashariki, Dar es Salaam akaandika ‘’Seminar Paper,’’ ‘’The Life of Kleist Sykes, ’’ (1968).

Mwalimu wake wa historia John Iliffe, aliitia ‘’paper,’’ hii kama sura moja katika kitabu alichohariri, ‘’Modern Tanzanians,’’ (1973). Nimeupitia mswada wa Kleist na kunyambua kile Waingereza wanakiita: ‘’War Dairies,’’ yaani Shajara za Vita, Kleist akieleza maisha yake katika Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 – 1918) akiwa askari katika jeshi la Wajerumani. Baadhi ya askari hawa kutoka Tanganyika walipigana katika vita hivi alikuwa ndugu yake Kleist, Schneider Abdillah Plantan ambae baadae alishiriki katika harakati za kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

***​

Miezi michache kabla Vita Vya Kwanza Vya Dunia haijaanza Ujerumani ilimteua Lettow-von Vorbeck kama Kamanda wa Majeshi ya Ulinzi ya Ujerumani katika Tanganyika. Askari wa zamani Waafrika waliopigana chini yake, pamoja na Kleist wanamkumbuka kwa mapenzi kama mtu mwema na askari shujaa. Kleist aliingizwa ndani ya jeshi la Wajerumani tarehe 13 November 1906 akiwa kijana mdogo sana wa umri miaka kumi na mbili na akapigana katika vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918). Katika jeshi Kleist alipata mafunzo ya mawasiliano. Baada ya miezi mitatu alihamishwa na kupelekwa Bataliani ya Pili kama karani katika Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam. Alibakia hapo hadi mwaka 1914. Vita vilipoanza, bataliani ya Kleist iliondoka Ukonga ikaelekea Mwakijembe, Tanga ambako kulikuwa na mashambulizi kutoka majeshi ya Waingereza kupitia mpaka wa Kenya. Katika bataliani hiyo alikuwapo Schneider, mtoto wa Affande Plantan.

Kleist alikuwa anazungumza Kijerumani na juu ya yote hayo alikuwa vilevile ni mtoto wa kulea wa Affande Plantan, kiongozi wa askari wa Kizulu katika utawala wa Wajerumani. Kwa ajili hii Kleist alipewa heshima ya pekee na akapewa nafasi kuwa mpambe wa von Lettow Vorbeck. Kumshuhudia kijana wa Kiafrika katika sare ya jeshi la Kijerumani akiongea Kijerumani huku anatembea nyuma ya von Lettow-Vorbeck, Mkuu wa Majeshi ya Wajerumani Tanganyika, bila shaka kuliwavutia wengi, hata Wajerumani wenyewe. Hii ilikuwa nafasi hasa iliyostahili mtoto wa askari ambae baba yake aliwasaidia Wajerumani kuiteka Tanganyika. Kama mpambe kazi yaje ilikuwa kushughulikia mambo yote ya Kamanda Mkuu. Alikuwa na jukumu la kuangalia chakula na usafi wa sare za von Lettow-Vorbeck, pamoja na mahitaji yake mengine. Alikuwa ndiye mtu wa kwanza Lettow-Vorbeck kukutananae asubuhi na wa mwisho kabla hajalala. Ilikuwa kazi yenye kumpa hadhi, mamlaka na heshima mbele ya askari wenzake. Utanashati wa Kleist katika mavazi na nidhamu yake katika maisha yake ya kawaida tu, yalitokana na kipindi hiki alichokuwa jeshini. Inaaminika kuwa hata ile hulka yake ya kuweka shajara na kuandika kumbukumbu muhimu ya mambo yake, yanatokana na uzoefu aliopata katika kipindi hiki akiwa jeshini. Inasemekana hii ndiyo miaka ambayo ilijenga silka na maisha ya Kleist.

Shajara zake za vita ni kielelezo binafsi kuhusu kampeni za Wajerumani na Waingereza wakati wa Vita Kuu Vya Kwanza. Shajara hizo zinaeleza kwa ukamilifu hali ya mambo yalivyokuwa kwa askari wa Kiafrika katika mapambano waliyoshiriki dhidi ya Waingereza. Kupitia maandishi ya Kleist unaweza ukaelewa ile chuki ambayo Waarabu walikuwanayo dhidi ya Wajerumani. Pambano la Kleist la kwanza dhidi ya Waarabu waliokuwa washirika wa Waingereza lilikuwa katika sehemu moja ijulikanayo kama Mwele Juu karibu ya Tanga.

Mbinu ya Lettow Vorbeck ilikuwa kuvuka mpaka wa Tanganyika na Kenya ili kukata mawasilano ya reli kati ya Mombasa na Kisumu. Reli hii ilikuwa jirani na mpaka wa Tanganyika. Ilikuwa mwendo wa siku chache kuifikia reli hii na kuikata Kenya na njia yake kuu kutoka Mombasa. Lakini jeshi la wanamaji wa Kiingereza lilikuwa Mombasa kwa hiyo bandari ya Mombasa ilikuwa imesalimika na manowari za Kijerumani. Ilikuwa wakati bataliani ya Kleist ipo Korogwe, mji uliopo maili chache kutoka Tanga, katika kijiji kiitwacho Semanya ndipo Kleist alipopokea habari kuwa Affande Plantan, baba yake Schneider na mlezi wake amefariki Dar es Salaam. Plantan alikuwa amekufa kwa homa ya matumbo tarehe 11 December 1914. Wajerumani walisimamisha vita kwa siku saba kwa heshima ya Affande Plantan.Wajerumani hawakuwa wezi wa fadhila walitambua kuwa alikuwa Affande Plantan waliekujanae kutoka Msumbiji kuja kuiteka Tanganyika. Alistahili kila aina ya heshima aliyostahili askari shujaa, hata kama alikuwa mamluki. Baada ya hapo Kleist na kamapani yake walielekea Tanga ambako kulikuwa makao makuu ya jeshi la Wajerumani wakati wa vita. Hapo hakukaa kwa muda mrefu kwa kuwa ilibidi kuomba likizo kurudi Dar es Salaam kumuangalia mama yake aliyekuwa mgonjwa. Alikaa Dar es Salaam kwa siku kumi akimuuguza mama yake kisha akarejea Tanga na akapewa kuongoza askari wanane katika divisheni ya kampani. Tarehe 24 December, 1915 kamapani yake iliamuriwa kwenda Mwakijembe na kisha Mwele Ndogo kuipokea 4th Reserve Company.

Waarabu walichukua nafasi hii ya msahambulizi ya Waingereza dhidi ya Wajerumani kulipiza kisasi dhidi yao. Waarabu waliungana na Waingereza kuwatimua Wajerumani Tanganyika. Bado baadhi yao walikuwa na kumbukumbu ya kitendo cha kikatili cha Wajeruani kwa shujaa wao Abushiri ambae walimnyonga mwaka 1889. Historia ikajirudia upya; Kleist na Schneider waliingia katika mapigano Mwele Ndogo dhidi ya adui wa zamani wa baba yao na adui wa Wajerumani ñ Waarabu. Mapambano haya yalifanyika siku ya mkesha wa Krismasi mwaka wa 1915 katika sehemu ile ile ambayo Sykes Mbuwane na Affande Plantan mamluki wa Kizulu waliteremka kwenye meli kuja kuwaongezea nguvu Wajerumani waliokuwa wakipigana na Waarabu na machifu wenyeji. Kwa saa kumi kuanzia alfajir hadi muda mchache kabla ya jua kuchwa, Wajerumani walibanwa katika mashambulizi makali. Kleist akapandishwa cheo na kuwa Lance Corporal kwa mchango wake katika pambano lile. Siku mbili baada ya pambano hilo Kleist na kampani yake waliamuriwa kwenda Kahe. Kleist Alibakia Kahe kwa mwezi mmoja kisha wakapata amri ya kwenda Voi,Kenya mji uliopo mpakani. Wakati wakiwa njiani kuelekea Voi, Kleist akaugua na ikabidi arudishwe Mombo, mji uliokuwa na mbu wengi kwa ajili ya mto uliokuwa unakatiza hapo mjini. Kleist alibaki akiugua hapo Mombo hospitalini kwa miezi miwili. Kutoka Mombo akaelekea Handeni. Mwezi Aprili 1916 habari zikamfikia bado akiwa katika uwanja wa mapambano kuwa mama yake amefariki dunia.

Mwaka wa 1916 Jeshi la Kiingereza lilikuja kuungwa mkono na askari kutoka Afrika ya Kusini walioshuka na meli Mombasa. Chini ya uongozi wa Jenerali Smutswalivuka mpaka wakaingia Tanganyika kupitia Namanga na Taveta. Haukupita muda mrefu mji wa Moshi ukatekwa. Batalioni ya Kleist ikawa sasa inarudi nyuma kuelekea Dodoma kulipokuwa na boma la Wajerumani. Si tu kuwa kikosi cha Kleist kilikuwa kinaandamwa na majeshi ya Waingereza, vikosi vya Wabelgiji navyo vilikuwa vimevuka mpaka kutoka Belgian Congo na kuingia Tanganyika. Wabelgiji waliteka Kigoma, Ujiji na Tabora. Mambo yalikuwa yamewachachia Wajerumani. Afya ya Kleist kwa wakati ule ikawa mbaya sana. Alifanyiwa uchunguzi Morogoro na akaonekana hawezi kuendelea kuitumikia katika kampeni yake. Afya yake haikumruhusu kupigana vita na ikabidi aachwe nyuma Mahenge wakati wenzake wakikimbia huku wakifukuzwa na adui. Kampani ya Kleist ilikwenda Chenene ambako walipambana kwa bunduki na vikosi vya Afrika ya Kusini kwa saa mbili. Kampani ile ikakimbilia Gode Gode, wakiponea chupu chupu. Kleist akakamatwa mateka mwezi Septemba 1917. Von Lettow Vorbeck mwishowe alifanikiwa kuvuka reli ya kati akavuka mpaka na kuingia Msumbiji, wakati huo ikijulikana kama Portuguese East Africa, akanusurika kutekwa yeye na askari wake. Kwa askari wa Kizulu hii ikawa ni nusra kwao kwa kuwa walikuwa wamerudishwa nyumbani.

Wakati von Lettow Vorbeck amefanikiwa kuponyoka kukamatwa, mpambe wake Kleist alitekwa na jeshi la Wabelgiji na wao wakamkabidhi kwa Waingereza. Waingereza walimtia Kleist kifungoni katika kambi ya mateka wa vita. Askari waliokuwa mateka pamoja na wagonjwa walichukuliwa na Waingereza na kutiwa kwenye kambi iliyokuwapo Kilosa. Kleist alikubali ukweli kuwa sasa yeye amepoteza hadhi yake kama askari, ni mateka, kwa hiyo akawa anasubiri hatima yake. Alibakia ndani yake kambi ile na yeye mwenyewe anaeleza katika kumbukumbu zake kuwa hakuwa na kinyongo chochote kwa maadui zake. Kleist aliweza hata kufanya urafiki na maadui zake ambao walikuwa wamemtia kifungoni. Kutokana na hali yake ya afya, Kleist hakuweza kufanya kazi zote za sulubu kama ilivyo desturi kwa wafungwa. Hali yake ya afya haikuwa inaonyesha dalili zozote za kupata nafuu, Kleist aliachiwa mwaka 1917 kwa hisia labda akiwa nje ya kambi, afya yake itarudi. Mwezi Novemba 1918 vita vikaisha huko Ulaya.
 
Simulizi ya kusisimua kweli. Mzee Mohamed Said, naomba uni tag utakapoweka sehemu inayofuata.
 
Bullet,
Hapo ndiyo mwisho lakini kama umependezewa na hii ngoja niingie Maktaba
nikuwekaa War Diaries za mwanae, Ally Sykes alipokuwa Burma WWII.
 
In 1943 we left Kilindini Harbour Mombasa in a convoy of ships heading for Ceylon escorted by the Royal Navy. African askaris were transported overseas from Mombasa escorted by the Royal Navy to ward off attacks from deadly Japanese submarines. We were first sent to Ceylon for jungle war training and to form the famous Burma Infantry to fight the Japanese. The Burma Infantry was formed by Africans from many countries including Northern Rhodesia (Zambia), Southern Rhodesia (Zimbabwe), Nyasaland (Malawi), Belgian Congo (Democratic Republic of Congo), Nigeria, Gold Coast (Ghana), Kenya, Uganda and Tanganyika and Zanzibar. Some of these African askaris had seen action in Abyssinia (Ethiopia) and Somaliland where the British and South Africans had engaged the Italians.

Owing to the successful campaign of this unit in Abyssinia there was an urgent need for pioneers. This was the reason behind the colonial government’s call for volunteers. African volunteers to the war effort were effective and decisive in the outcome of the war.

While our convoy was sailing towards Colombo one of the ships was torpedoed by a Japanese submarine. The vessel sank, killing all African askaris and our white officers on board. Only one askari from Tanga known as Magembe survived. We were not informed about the tragedy until upon our arrival in Colombo. The white officers thought if we were to be informed about the tragedy while still in the high seas there would be general panic which would have been bad for morale. The army bulletin Second Echelon, published weekly and circulated among military camps of the allied forces, published my name and number by mistake as among those who had perished at sea.

Abdulwahid learnt of my ‘death’ from the bulletin and he in turn communicated the sad news to my father back home. Prayers for the departed were read for me at the mosque near our house. The mosque still stands today although not in its original form. The old small mosque has now been replaced by a storey building. I can only imagine the sorrow of my parents much as I can imagine their happiness when they were told I was alive and well.
 
Bullet,
Hapo ndiyo mwisho lakini kama umependezewa na hii ngoja niingie Maktaba
nikuwekaa War Diaries za mwanae, Ally Sykes alipokuwa Burma WWII.

Oh kumbe imefika mwisho. Whoever wrote it is such a good orator! Nitasubiri hizo za wanae. Asante mzee.
 
Mwandishi ni mimi nikisaidiana na Ally Sykes.
Hujasoma kitabu changu?

1542137727293.png
 
Bullet,
Mwandishi ni mimi nikisaidiana na Ally Sykes.
Hujasoma kitabu changu?

Kitabu nilikisoma pindi tu kilipotoka, ila kuna mtu nilimuazima na bahati mbaya nikamsahau na yeye hakunikumbusha hivyo nikakipoteza. Ila nilishakisoma muda mrefu tu.
 
Bullet,
Naamini ulikutana na mengi katika kitabu yaliyokushangaza.
Ally Sykes anaendelea kueleza:

''At Kurunegala, we Africans underwent jungle training for four months before sailing to Burma from Trincomalee via Chittagong in present-day Bangladesh. All the time we sailed in convoy escorted by the British Royal Navy moving slowly, keeping to safe waters, always on the lookout for Japanese attack.

It was at Chittagong where we got the first taste of what the Burma infantry had in store for us. There was a distance of about ten km between the harbour and the camp. The road was rough and always covered with mud which was ankle deep due to heavy monsoon rains. The camp was dirty with mud all over the place. Each one of us had to carry his heavy luggage to the camp. We had kitbag, haversack, gun and bullets. We also had to dig trenches that very day for ourselves and for our white officers. The camp gave an indication to the African askari of what we would have to endure even before we had even been shot at by the Japanese.

We were considered ‘military labour,’ while whites such as Americans and New Zealanders were identified as ‘allies’. These semantics were probably not lost upon us. By being termed ‘military labour,’ we were reduced to muscle force without brains, to be used to accomplish a difficult task. We were labelled as ‘natives’ and were classified into English-speaking and non English-speaking. A British soldier’s salary was much higher than one drawn by an African of the same rank.

Even food was categorized according to race. There was a European, an Asian and an African diet; African diet being the poorest. A British soldier was provided with what was known as ‘family allotment allowance’ to support his family back home. There was no such allowance for Africans. Africans were given rum as part of their diet while whites were provided with brandy, whisky and beer.''
 
kama nasikia sauti ya msimuliaji vile.kaka uko vizuri.
 
Thanks mzee wetu mohamed said kw nukta muhim na shahara yeny kutup faida ambawo tulikuw hatufaham awali hawa watu shukrn san
 
SHAJARA ZA VITA ZA LANCE CORPORAL KLEIST SYKES
(1894 - 1949)

VITA VYA KWANZA VYA DUNIA 1914- 1918

Utangulizi

November 11, 1918 ndiyo siku Vita Vya Kwanza Vya Dunia vilimazilizika na dunia inaadhimisha siku hii.

Kleist Sykes hajaacha kunishangaza kila ninapoyaangalia maisha yake kupitia mswada alioandika kabla hajafa mwaka wa 1949 mswada ambao alimwachia mwanae Abdul Sykes na yeye Abdul akampa binti yake Aisha Daisy Sykes na Daisy akiwa mwanafunzi wa Historia Chuo Kikuu Cha Afrika Mashariki, Dar es Salaam akaandika ‘’Seminar Paper,’’ ‘’The Life of Kleist Sykes, ’’ (1968).

Mwalimu wake wa historia John Iliffe, aliitia ‘’paper,’’ hii kama sura moja katika kitabu alichohariri, ‘’Modern Tanzanians,’’ (1973). Nimeupitia mswada wa Kleist na kunyambua kile Waingereza wanakiita: ‘’War Dairies,’’ yaani Shajara za Vita, Kleist akieleza maisha yake katika Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 – 1918) akiwa askari katika jeshi la Wajerumani. Baadhi ya askari hawa kutoka Tanganyika walipigana katika vita hivi alikuwa ndugu yake Kleist, Schneider Abdillah Plantan ambae baadae alishiriki katika harakati za kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

***​

Miezi michache kabla Vita Vya Kwanza Vya Dunia haijaanza Ujerumani ilimteua Lettow-von Vorbeck kama Kamanda wa Majeshi ya Ulinzi ya Ujerumani katika Tanganyika. Askari wa zamani Waafrika waliopigana chini yake, pamoja na Kleist wanamkumbuka kwa mapenzi kama mtu mwema na askari shujaa. Kleist aliingizwa ndani ya jeshi la Wajerumani tarehe 13 November 1906 akiwa kijana mdogo sana wa umri miaka kumi na mbili na akapigana katika vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918). Katika jeshi Kleist alipata mafunzo ya mawasiliano. Baada ya miezi mitatu alihamishwa na kupelekwa Bataliani ya Pili kama karani katika Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam. Alibakia hapo hadi mwaka 1914. Vita vilipoanza, bataliani ya Kleist iliondoka Ukonga ikaelekea Mwakijembe, Tanga ambako kulikuwa na mashambulizi kutoka majeshi ya Waingereza kupitia mpaka wa Kenya. Katika bataliani hiyo alikuwapo Schneider, mtoto wa Affande Plantan.

Kleist alikuwa anazungumza Kijerumani na juu ya yote hayo alikuwa vilevile ni mtoto wa kulea wa Affande Plantan, kiongozi wa askari wa Kizulu katika utawala wa Wajerumani. Kwa ajili hii Kleist alipewa heshima ya pekee na akapewa nafasi kuwa mpambe wa von Lettow Vorbeck. Kumshuhudia kijana wa Kiafrika katika sare ya jeshi la Kijerumani akiongea Kijerumani huku anatembea nyuma ya von Lettow-Vorbeck, Mkuu wa Majeshi ya Wajerumani Tanganyika, bila shaka kuliwavutia wengi, hata Wajerumani wenyewe. Hii ilikuwa nafasi hasa iliyostahili mtoto wa askari ambae baba yake aliwasaidia Wajerumani kuiteka Tanganyika. Kama mpambe kazi yaje ilikuwa kushughulikia mambo yote ya Kamanda Mkuu. Alikuwa na jukumu la kuangalia chakula na usafi wa sare za von Lettow-Vorbeck, pamoja na mahitaji yake mengine. Alikuwa ndiye mtu wa kwanza Lettow-Vorbeck kukutananae asubuhi na wa mwisho kabla hajalala. Ilikuwa kazi yenye kumpa hadhi, mamlaka na heshima mbele ya askari wenzake. Utanashati wa Kleist katika mavazi na nidhamu yake katika maisha yake ya kawaida tu, yalitokana na kipindi hiki alichokuwa jeshini. Inaaminika kuwa hata ile hulka yake ya kuweka shajara na kuandika kumbukumbu muhimu ya mambo yake, yanatokana na uzoefu aliopata katika kipindi hiki akiwa jeshini. Inasemekana hii ndiyo miaka ambayo ilijenga silka na maisha ya Kleist.

Shajara zake za vita ni kielelezo binafsi kuhusu kampeni za Wajerumani na Waingereza wakati wa Vita Kuu Vya Kwanza. Shajara hizo zinaeleza kwa ukamilifu hali ya mambo yalivyokuwa kwa askari wa Kiafrika katika mapambano waliyoshiriki dhidi ya Waingereza. Kupitia maandishi ya Kleist unaweza ukaelewa ile chuki ambayo Waarabu walikuwanayo dhidi ya Wajerumani. Pambano la Kleist la kwanza dhidi ya Waarabu waliokuwa washirika wa Waingereza lilikuwa katika sehemu moja ijulikanayo kama Mwele Juu karibu ya Tanga.

Mbinu ya Lettow Vorbeck ilikuwa kuvuka mpaka wa Tanganyika na Kenya ili kukata mawasilano ya reli kati ya Mombasa na Kisumu. Reli hii ilikuwa jirani na mpaka wa Tanganyika. Ilikuwa mwendo wa siku chache kuifikia reli hii na kuikata Kenya na njia yake kuu kutoka Mombasa. Lakini jeshi la wanamaji wa Kiingereza lilikuwa Mombasa kwa hiyo bandari ya Mombasa ilikuwa imesalimika na manowari za Kijerumani. Ilikuwa wakati bataliani ya Kleist ipo Korogwe, mji uliopo maili chache kutoka Tanga, katika kijiji kiitwacho Semanya ndipo Kleist alipopokea habari kuwa Affande Plantan, baba yake Schneider na mlezi wake amefariki Dar es Salaam. Plantan alikuwa amekufa kwa homa ya matumbo tarehe 11 December 1914. Wajerumani walisimamisha vita kwa siku saba kwa heshima ya Affande Plantan.Wajerumani hawakuwa wezi wa fadhila walitambua kuwa alikuwa Affande Plantan waliekujanae kutoka Msumbiji kuja kuiteka Tanganyika. Alistahili kila aina ya heshima aliyostahili askari shujaa, hata kama alikuwa mamluki. Baada ya hapo Kleist na kamapani yake walielekea Tanga ambako kulikuwa makao makuu ya jeshi la Wajerumani wakati wa vita. Hapo hakukaa kwa muda mrefu kwa kuwa ilibidi kuomba likizo kurudi Dar es Salaam kumuangalia mama yake aliyekuwa mgonjwa. Alikaa Dar es Salaam kwa siku kumi akimuuguza mama yake kisha akarejea Tanga na akapewa kuongoza askari wanane katika divisheni ya kampani. Tarehe 24 December, 1915 kamapani yake iliamuriwa kwenda Mwakijembe na kisha Mwele Ndogo kuipokea 4th Reserve Company.

Waarabu walichukua nafasi hii ya msahambulizi ya Waingereza dhidi ya Wajerumani kulipiza kisasi dhidi yao. Waarabu waliungana na Waingereza kuwatimua Wajerumani Tanganyika. Bado baadhi yao walikuwa na kumbukumbu ya kitendo cha kikatili cha Wajeruani kwa shujaa wao Abushiri ambae walimnyonga mwaka 1889. Historia ikajirudia upya; Kleist na Schneider waliingia katika mapigano Mwele Ndogo dhidi ya adui wa zamani wa baba yao na adui wa Wajerumani ñ Waarabu. Mapambano haya yalifanyika siku ya mkesha wa Krismasi mwaka wa 1915 katika sehemu ile ile ambayo Sykes Mbuwane na Affande Plantan mamluki wa Kizulu waliteremka kwenye meli kuja kuwaongezea nguvu Wajerumani waliokuwa wakipigana na Waarabu na machifu wenyeji. Kwa saa kumi kuanzia alfajir hadi muda mchache kabla ya jua kuchwa, Wajerumani walibanwa katika mashambulizi makali. Kleist akapandishwa cheo na kuwa Lance Corporal kwa mchango wake katika pambano lile. Siku mbili baada ya pambano hilo Kleist na kampani yake waliamuriwa kwenda Kahe. Kleist Alibakia Kahe kwa mwezi mmoja kisha wakapata amri ya kwenda Voi,Kenya mji uliopo mpakani. Wakati wakiwa njiani kuelekea Voi, Kleist akaugua na ikabidi arudishwe Mombo, mji uliokuwa na mbu wengi kwa ajili ya mto uliokuwa unakatiza hapo mjini. Kleist alibaki akiugua hapo Mombo hospitalini kwa miezi miwili. Kutoka Mombo akaelekea Handeni. Mwezi Aprili 1916 habari zikamfikia bado akiwa katika uwanja wa mapambano kuwa mama yake amefariki dunia.

Mwaka wa 1916 Jeshi la Kiingereza lilikuja kuungwa mkono na askari kutoka Afrika ya Kusini walioshuka na meli Mombasa. Chini ya uongozi wa Jenerali Smutswalivuka mpaka wakaingia Tanganyika kupitia Namanga na Taveta. Haukupita muda mrefu mji wa Moshi ukatekwa. Batalioni ya Kleist ikawa sasa inarudi nyuma kuelekea Dodoma kulipokuwa na boma la Wajerumani. Si tu kuwa kikosi cha Kleist kilikuwa kinaandamwa na majeshi ya Waingereza, vikosi vya Wabelgiji navyo vilikuwa vimevuka mpaka kutoka Belgian Congo na kuingia Tanganyika. Wabelgiji waliteka Kigoma, Ujiji na Tabora. Mambo yalikuwa yamewachachia Wajerumani. Afya ya Kleist kwa wakati ule ikawa mbaya sana. Alifanyiwa uchunguzi Morogoro na akaonekana hawezi kuendelea kuitumikia katika kampeni yake. Afya yake haikumruhusu kupigana vita na ikabidi aachwe nyuma Mahenge wakati wenzake wakikimbia huku wakifukuzwa na adui. Kampani ya Kleist ilikwenda Chenene ambako walipambana kwa bunduki na vikosi vya Afrika ya Kusini kwa saa mbili. Kampani ile ikakimbilia Gode Gode, wakiponea chupu chupu. Kleist akakamatwa mateka mwezi Septemba 1917. Von Lettow Vorbeck mwishowe alifanikiwa kuvuka reli ya kati akavuka mpaka na kuingia Msumbiji, wakati huo ikijulikana kama Portuguese East Africa, akanusurika kutekwa yeye na askari wake. Kwa askari wa Kizulu hii ikawa ni nusra kwao kwa kuwa walikuwa wamerudishwa nyumbani.

Wakati von Lettow Vorbeck amefanikiwa kuponyoka kukamatwa, mpambe wake Kleist alitekwa na jeshi la Wabelgiji na wao wakamkabidhi kwa Waingereza. Waingereza walimtia Kleist kifungoni katika kambi ya mateka wa vita. Askari waliokuwa mateka pamoja na wagonjwa walichukuliwa na Waingereza na kutiwa kwenye kambi iliyokuwapo Kilosa. Kleist alikubali ukweli kuwa sasa yeye amepoteza hadhi yake kama askari, ni mateka, kwa hiyo akawa anasubiri hatima yake. Alibakia ndani yake kambi ile na yeye mwenyewe anaeleza katika kumbukumbu zake kuwa hakuwa na kinyongo chochote kwa maadui zake. Kleist aliweza hata kufanya urafiki na maadui zake ambao walikuwa wamemtia kifungoni. Kutokana na hali yake ya afya, Kleist hakuweza kufanya kazi zote za sulubu kama ilivyo desturi kwa wafungwa. Hali yake ya afya haikuwa inaonyesha dalili zozote za kupata nafuu, Kleist aliachiwa mwaka 1917 kwa hisia labda akiwa nje ya kambi, afya yake itarudi. Mwezi Novemba 1918 vita vikaisha huko Ulaya.
 
Naomba uwe wanitag kila utakapo gusia au kuwek kuhus histora halisi na kila jambo mzee wetu
 
Back
Top Bottom