SWEETIE PIE
New Member
- Jul 25, 2022
- 1
- 0
Mwili wa binaadamu hujengwa kwa vyakula na lishe bora ya kiasili isiyo na kemikali ikiwemo kula mboga mboga, kunywa maji kwa wingi, kula matunda, kula vyakula visivyokua na mafuta mengi, kula vyakula visivyokua na sukari nyingi, mlo wenye mpangilio maalumu, kuachana na kupunguza vyakula vyenye kemikali nyingi kama vile chipsi, soseji, kuku wa peduu, soda na kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zetu. Mazoezi yanaweza kubadilisha afya yako na kua na muonekano imara na wa kupendeza endapo utayafanya ipasavyo. Dhana ya mazoezi nchini Tanzania na nchi nyenginezo duniani inahitaji kukuzwa na kubadilishwa ili kusaidia jamii kuboresha afya zetu. Baadhi ya watu hudhani kua mazoezi ni kwa ajili ya kupunguza mwili tu na pia wengine bado husema kua mazoezi ni kwa wanaume tu, na wengine husema kua mazoezi yananenepesha mwili.
Wanawake wengi huogopa kufanya mazoezi kwa kudhani kua lazima watoke nje uwanjani kila mtu anakuona hali ya kua ni ngumu sana kufanya hivyo hasa kwa wanawake waliokua na familia na ni walezi wa Watoto wao wenyewe, kutokana na majukumu mengi ya kazi za nyumbani na pirika za kiuchumi , na baadhi yao huona aibu kufanya mazoezi mbele za watu. Na wengine husema kua mazoezi yanaumiza sana mwili na yanataka utumie sana nguvu, yaani mazoezi ni kitu kigumu sana na hawawezi kufanya na kudumu nayo. Hizi fikra zina ukweli ndani yake kutokana na kukosa uelewa na motisha kuhusiana na umuhimu wa mazoezi kwa binaadamu na namna ya kufanya mazoezi.
Hapa nazungumzia zaidi wanawake kwa sababu ni wahanga wakuu wa kutumia mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanapata muonekano mzuri wa miili yao. Wanawake wengi hutumia vidonge, dawa za kunywa, sindano au krimu za kujipaka kwa ajili ya kupunguza matiti, tumbo , kuchonga uso au kuongeza makalio. Na wanawake wengine hupasua miili yao kwa kufanya (surgery) ili kuweza kuwa na mwili wautakao. Kiafya yote haya sio salama na yana athari sana kwa Maisha ya binaadamu na athari hizo ni za kuonekana na nyengine sio za kuonekana kiharaka ambazo sio nzuri kwa maisha ya mwanaadamu na kupelekea kansa na maradhi mengine hatarishi. Endapo wanawake watafanya mazoezi ipasavyo kwa kuzingatia masharti na aina ya mazoezi wanaweza kua na miili waipendayo. Mazoezi ya kutengeneza shepu au kuweka miili katika hali nzuri ni kama yafuatayo: -
Aina ya mazoezi maalumu kwa wanawake kuweka mwili upendavyo: -
Mazoezi ya kupunguza tumbo (Kegel exercise).
Mazoezi ya kuondoa nyama zembe za mgongoni.
Mazoezi ya kupunguza nyama za uso na shingo. (Yoga).
Mazoezi ya kuongeza na kuinua makalio. (Squats).
Mazoezi ya kubana uke Kwa mama waliojifungua.
Mazoezi ya kusimamisha matiti.
Mazoezi ya kuondoa msongo wa mawazo.
Mazoezi ya kupunguza nyama za mikono na miguu.
Mazoezi ya kupunguza uzito mwili mzima.
Mazoezi ya kuongeza mwili.
Mazoezi ya wajawazito.
Nini kifanyike ili watu hususani wanawake waweze kua na mazowea na uelewa wa faida za mazoezi?
Kuna umuhimu sana wa kufanya mazoezi kwa kila binaadamu kuanzia Watoto, wanaume, wanawake, watu wenye ulemavu na watu wazima kwa ajili ya kuweka afya imara na ustawi bora wa Maisha yetu. Mazoezi ni muhimu sana kwa sababu yanasaidia mwili kua na nguvu, kuchelewa kuzeeka, kuipa nywele, Ngozi na akili afya, kuimarisha ubongo kuwa na kumbukumbu, kuimarisha mifupa, kuepukana na msongo wa mawazo kwa kukufanya kuwa na furaha na pia kusaidia kujikinga na maradhi hatarishi kama vile kansa. Hivyo basi ni wajibu wa kila binaadamu kufatilia jinsi ya kufanya mazoezi kwa afya na kwa kuweka mwili sawa kupitia wakufunzi wazoefu wa mazoezi mbali mbali katika jamii zetu. Na kwa ambao tayari wanafanya mazoezi ni vizuri kuendelea kuyafanya ili kuimarisha afya na kujenga jamii yenye ustawi mzuri na kuchangia kutimiza malengo endelevu ya dunia ambapo lengo nambari tatu ni kuwa na afya bora na ustawi mzuri duniani. Kwa kuchangia afya bora tuanze kuwa na msingi mzuri kuanzia chakula tunachokula na vitu ambavyo tunatumia na pia kufanya mazoezi na kuelimisha wengine ili tuwe na jamii yenye afya bora na kusaidia maendeleo nchini Tanzania na duniani kiujumla.
VYANZO VYA PICHA:
download kegel exercise pictures - Bing images
download pregnant exercise pictures - Bing images
download body weight squat exercise pictures - Bing images

- Elimu ya msingi: Kuanzia mashuleni hadi majumbani watoto waweze kushirikishwa kwenye michezo mbali mbali na mashindano, mfano mpira wa miguu, nage , tae- kon- do, yoga,kick boxing, mbio za miguu, sarakasi n.k, ili kuuwezesha mwili kupenda mazoezi kua imara na itakua ni njia rahisi kuanzia utotoni ili kujenga mazowea ya kila siku.
- Vituo vya kufanyia mazoezi kwa wanawake tu: Kuna vituo vingi tu vya wanaume mfano gym kwa ajili ya kujenga misuli. Lakini kunahitajika ongezeko la vituo vya wanawake ili kuweza kuwajengea kujiamini na kupenda mazoezi. Nchini Zanzibar, Tanzania kwa mfano kituo cha wanawake kinachoitwa wajamama WAJAMAMA na vyenginevyo kwa ajili ya wanawake tu kufanya mazoezi.
- Kufanya mazoezi nyumbani: Endapo wanawake hawatoweza kujiunga na vikundi au vituo tofauti vya mazoezi, basi wanaweza kufanya mazoezi wakiwa nyumbani kwao Pamoja na wenza wao na Watoto wao kwa kutumia vifaa maalumu kama vile mikeka maalumu ili wasiumie mgongo, mikanda, baiskeli, Kamba za kuruka, mipira, viringi na vyenginevyo. Pia kujiwekea ratiba angalau kufanya zoezi kwa wiki mara mbili au tatu kulingana na mda wako.
- Kujifunza mitandaoni: Kujifunza kupitia youtube, Instagram bure kwa kuangalia video za wakufunzi mbali mbali kama vile, ‘womens workout channel’ (207) Womens Workout Channel - YouTube n.k.

Upvote
1