BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
SHAKA AKAGUA MIRADI PEMBA, AAHIDI CCM ITAWALINDA WABUNGE ,WAWAKILISHI NA MADIWANI.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amekagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kisiwani Pemba na kuwahakikishia wananchi kuwa Chama kitaendelea kuwalinda wabunge , Wawakilishi na madiwani wake wanaotekeleza ahadi zao.
Akiwa katika ziara hiyo iliyoanza jana visiwani humo, Shaka amekagua miradi ya madarasa na kisima cha maji safi na salama katika Jimbo la Gando, miradi ambayo imewapunguzia adha wananchi ikiwemo ya kufuata maji umbali mrefu.
Akizungumza katika mkutano wa Mbunge wa Jimbo hilo,uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira Kizimbami Shaka amesema utekelezaji wa Miradi ya maendeleo unaofanyika katika Jimbo hilo na maeneo mengine yanayoongozwa na wabunge na madiwani wa CCM.
Shaka amesema utekelezaji wa Miradi unaofanywa na viongozi wa CCM unalenga kutekeleza ahadi na kutatua changamoto za wananchi katika huduma za jamii ikiwemo afya, elimu na maji.
Aidha, Shaka amewahakikishia wabunge na madiwani wanaotokana na CCM kwamba Chama kitaendelea kuwalinda dhidi ya yeyote anayetaka kuwavuruga na kusababisha washindwe kutekeleza majukumu yao.
Amesema wabunge na madiwani wanapaswa kuachwa watekeleze Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba mwanachama yeyote mwenye malengo ya kuomba uongozi asubiri wakati mwafaka unaoruhusiwa kisheria.
Awali baada ya kuwasili kisiwani humo, Shaka alizuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Dk. Omari Ali Juma, wilayani Chakechake na baadae kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar marehemu Maalim Seif Sharif Hamad lililopo Kijiji cha Mnyali, Mtambwe wilaya ya Were Mkoa wa Kaskazini Pemba.
=== ===