KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA, ITIKADI NA UENEZI SHAKA HAMDU SHAKA, ATUA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Shaka Hamdu Shaka Jumanne
26 Oktoba, 2021 ametembelea Ofisi za Bodi ya Mikopo ya wanafunzi elimu ya Juu zilizopo maeneo ya Tazara Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na viongozi na watendaji wa bodi hiyo.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeielekeza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuendelea kutoa kipaumbele kwa kundi la watoto masikini na wenye mahitaji maalumu wenye vigezo vya kunufaika.
Pia, kimeipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuwafikia wanafunzi, huku ikisema ongzeko la marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika kulikotokana na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kufuta Kodi ya ongezeko la zuio kwenye Mikopo ya elimu ya Juu (Retention fee), ni kielelezo cha ufanisi.
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, alipotembelea HESLB kuona jinsi inavyofanya kazi.
Shaka alieleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ibara ya 80 (h) inasema serikali itaimarisha na kuboresha mfumo wa ugharimiaji wa elimu ya juu ikiwemo bodi ya mikopo ya Juu, ili kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wenye uhitaji na sifa stahiki wanapata fursa ya kujiunga na elimu ya juu.
Alisema Rais Samia ameonyesha dhamira ya dhati kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kusoma ambapo, ameongeza mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka sh bilioni 464 hadi sh. bilioni 570.
#ChamaImara
#KaziIendee