Shaka atumia Kijiwe cha Kahawa Tabora kuelezea Mwelekeo wa Rais katika Kilimo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
SHAKA ATUMIA KIJIWE CHA KAHAWA TABORA KUELEZA MWELEKEO WA RAIS KATIKA KILIMO

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, (NEC) ya CCM, tikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ametembelea kijiwe cha Kahawa Lumumba kilichopo Tabora Mjini na kunywa kahawa na wananchi na kutumia fursa hiyo kuelezea hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuimarisha sekta ya kilimo.

Akiwa kijiweni hapo, Shaka alitoa nafasi ya kusikiliza wananchi hao ambao walitoa pongezi kwa Rais Samia na Chama Cha Mapinduzi kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuleta maendeleo na kusimamia utekelezaji wa Ilani.

Aidha, wananchi hao walimuombia Shaka kufikisha salamu zao kwa Rais Samia wakimuomba aendelee kuongeza fedha katika sekta ya kilimo ambayo Watanzania wengi wanakitumia kama shughuli rasmi ya kujipatia kipato.

Pia, waliomba kupunguzwa kwa gharama ya maji ambayo wameeleza ni kubwa mjini Tabora.

Akizungumza Shaka ameelezea hatua kwa hatua kuhusu mipango inayoendelea kutekelezwa na serikali ya Rais Samia kuhakikisha maendeleo yanafika maeneo yote huku akieleza pia kuhusu juhudi za kuboresha kilimo.

“Rais Samia kwa kutambua umuhimu wa sekta ya kilimo ameendelea kuchukua hatua mbalimbali na miongoni mwa hatua hizo ni kuongeza fedha katika bajeti ya kilimo kutoka Sh. bilioni 254 hadi sh. bilioni 999. Ni ongezeko kubwa na ataendelea kuongeza kidogo kidogo hadi mambo yatakuwa sawa,” alisema.

Kuhusu changamoto ya bei kubwa ya ulipaji maji kwa wananchi wa Tabora Mjini, Shaka amesema atalifikisha suala hilo kwa Waziri wa Maji Jumma Aweso kuona hatua gani zinaweza kuchukuliwa kupunguza bei ya maji kama ambavyo wananchi wanaona.

IMG-20220817-WA0171.jpg

IMG-20220817-WA0173.jpg
IMG-20220817-WA0169.jpg

IMG-20220817-WA0170.jpg
 
Kuna makada wa chama fulani walitumia vijiwe kama hivi kuelezea sera za chama Chao waliambulia kukamatwa na polisi na kipigo ila upande huu mambo Shwari.

Tuache ubaguzi wa vyama, kila chama kipewe haki ya kufanya siasa.
Erythrocyte
 
SHAKA ATUMIA KIJIWE CHA KAHAWA TABORA KUELEZA MWELEKEO WA RAIS KATIKA KILIMO

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, (NEC) ya CCM, tikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ametembelea kijiwe cha Kahawa Lumumba kilichopo Tabora Mjini na kunywa kahawa na wananchi na kutumia fursa hiyo kuelezea hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuimarisha sekta ya kilimo.

Akiwa kijiweni hapo, Shaka alitoa nafasi ya kusikiliza wananchi hao ambao walitoa pongezi kwa Rais Samia na Chama Cha Mapinduzi kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuleta maendeleo na kusimamia utekelezaji wa Ilani.

Aidha, wananchi hao walimuombia Shaka kufikisha salamu zao kwa Rais Samia wakimuomba aendelee kuongeza fedha katika sekta ya kilimo ambayo Watanzania wengi wanakitumia kama shughuli rasmi ya kujipatia kipato.

Pia, waliomba kupunguzwa kwa gharama ya maji ambayo wameeleza ni kubwa mjini Tabora.

Akizungumza Shaka ameelezea hatua kwa hatua kuhusu mipango inayoendelea kutekelezwa na serikali ya Rais Samia kuhakikisha maendeleo yanafika maeneo yote huku akieleza pia kuhusu juhudi za kuboresha kilimo.

“Rais Samia kwa kutambua umuhimu wa sekta ya kilimo ameendelea kuchukua hatua mbalimbali na miongoni mwa hatua hizo ni kuongeza fedha katika bajeti ya kilimo kutoka Sh. bilioni 254 hadi sh. bilioni 999. Ni ongezeko kubwa na ataendelea kuongeza kidogo kidogo hadi mambo yatakuwa sawa,” alisema.

Kuhusu changamoto ya bei kubwa ya ulipaji maji kwa wananchi wa Tabora Mjini, Shaka amesema atalifikisha suala hilo kwa Waziri wa Maji Jumma Aweso kuona hatua gani zinaweza kuchukuliwa kupunguza bei ya maji kama ambavyo wananchi wanaona.

View attachment 2326442
View attachment 2326444View attachment 2326445
View attachment 2326446
Hakuna anayemwelewa hapo, jibu wanalo moyoni hao wanaomsikiliza watatenda kwa wakati wake
 
Hii ndio maana halisi ya chama kiongozi, CCM ndio Tumaini la wananchi katika kuwaletea maendeleo, CCM ndio maskio ya wananchi, CCM ndio mdomo wa wananchi wanyonge wasioweza kupaza sauti zao zikasikika,

CCM inashuka na kwenda kuwafuata wananchi waliko na kuwasikiliza,maana inatambua kuwa wao ndio mabosi na ndio wanaotakiwa kutumikiwa kwa kusikilizwa kero zao na kuzitafutia majibu na suluhisho la kudumu

CCM itaendeleaa kupewa dhamani ya kuongoza nchi hii uchaguzi Hadi uchaguzi kwa kuwa chama kimeendelea kupewa na kuaminika na wananchi, CCM Ni sikivu na inaisimamia serikali iliyoiunda ili kuhakikisha kuwa inafanya kazi zinazogusa maisha ya watu,
 
Watu waliomo kwenye hicho chama sio viongozi ni wafanyabiashara kwa migongo ya wananchi hawafai
 
Back
Top Bottom