SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Na Mwandishi Wetu,
Kutoka Tanga.
-Wataka Rais Samia Asishinikizwe kukutana nao
Mwandishi wetu Tanga.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza kitaendelea kutoa mwelekeo wa siasa na uongozi wa nchi kwa vile ndicho kinachounda na kuongoza serikali, hivyo viongozi wa Chama na serikali katika ngazi za Kijiji hadi taifa kwa kiasi kikubwa wote wako katika fatiki za kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ili kutimiza wajibu wake kwa wananchi kwa kuwaondoshea kero na changamoto mbalimbali ili kuharakisha maendeleo.
Kimesema wakati wote Chama cha Mapinduzi kimekuwa chenye dhamira chanya ya kutoshiriki siasa za mti kwa macho, piga nikupige, kuhasimiana kisiasa na kuwagawa wananchi kwa sababu zozote zile, hivyo mwelekeo wake ni kuhimiza siasa safi zinazojali ustawi wa haki, usawa, amani, usalama, umoja na mshikamano na kusimamia maslahi ya wananchi walio wengi.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo wakati akizungumza na na wanachi wa Pangani Magharibi mkoani hapa ambapo alisema bado baadhi ya matamko ya viongozi wa upizani hayana afya katika ujenzi wa umoja wa kitaifa hasa kipindi hichi ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amejipambanua katika kuwatumikia watanzania bila kuwabagua kwa misingi ya itikadi zao za kisiasa, ukanda, ukabila au udini.
“Matamshi yaliyotamkwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa hivi karibuni yamevuka mipaka huku yakiwathibitishia watanzania kuwa baadhi ya vyama hivyo hakuna wanasiasa wenye maarifa na upeo, wenye kutambua dhana ya mgawanyo wa madaraka, wala kuelewa mipaka ya utawala pia yaonesha hawafahamu hadhi, nguvu wala dhamana ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanai Samia Suluhu Hassan” Alisema Shaka
Shaka amefafanua kuwa hakuna chama chochote cha siasa chenye wajibu wala haki ya kumuamrisha Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama au kutoa shinikizo la aina yoyote Zaidi ya kuheshimiwa maamuzi yake anapoataka nani amuone lini ama kwa muda gani na si kwa madai ya kuandika barua na kuchelewa wahusika kupata majibu.
“Hakuna sababu ya kutishana wala kutoa masharti na shinikizo kwa jambo lolote lile kwani ni Rais Samia kwa kuthamini kwake ushirikishwaji wa kila mmoja wetu katika ujenzi wa nchi yetu akaona atafakari ni wakati gani akutane na viongozi wote wa vyama vya siasa sasa wasitake kujifanya ni wao ndio walitaka hilo. Aidha wapo viongozi wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa mahiri wa kuchonga, kuzua na kuzusha mambo yanayopotosha, yanayochochea chuki na hata kuathiri umoja na mshikamano wetu lengo lao likiwa ni kutaka kututoa Chama na serikali kwenye mwelekeo wa ujenzi wa nchi yetu na tuanze malumbano nao jambo ambalo kamwe hawatafanikiwa zaidi tutawapa elimu ya siasa safi, uongozi na uzalendo kutokana na viongozi hao kuonekana wamekosa malezi mazuri ya kiuongozi au wamekosa kazi za kufanya.” Alisema Shaka
Shaka yuko katika ziara ya kikazi mkoani Tanga ambapo ataendelea na ziara yake katika wilaya za Muheza na Tanga Mjini. Ziara hiyo inaongozwa na katibu mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo ambaye yupo wilaya za Kilindi, Handeni na Korogwe. Wameongozana pia na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ndugu Ngemela Lubinga ambaye atapita wilaya za Mkinga, Lushoto na Bumbuli.