CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, imempitisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea uenyeki wa CCM katika uchaguzi wa Chama utakaofanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC kilichoketi leo Desemba 6, 2022 Shaka ameema pamoja na mambo mengine kilipitia na kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi mbalimbali.
Shaka amesema mbali na Dk. Samia, pia NEC imewapitisha Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana kuwa mgombea umakamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (Zanzibar) huku pia kikipitisha wagombea wa Viti 30 vya huku kila upande wa Muungano ukiwa na nafasi 15.