Shaka: CCM imetimia kazi inaendelea. Maandalizi ya Mkutano Mkuu yamefikia 99%, wajumbe tembeeni vifua mbele

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

Your browser is not able to display this video.


Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, imempitisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea uenyeki wa CCM katika uchaguzi wa Chama utakaofanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dodoma.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC kilichoketi leo Desemba 6, 2022 Shaka ameema pamoja na mambo mengine kilipitia na kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi mbalimbali.

Shaka amesema mbali na Dk. Samia, pia NEC imewapitisha Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana kuwa mgombea umakamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (Zanzibar) huku pia kikipitisha wagombea wa Viti 30 vya huku kila upande wa Muungano ukiwa na nafasi 15.

 
Moja ya sifa kuu ya CCM ni kubadilika badilika na Ndio sababu huwa nasema CCM itatawala miaka mingi Sana kwakuwa inajua kushughulika na matatizo ya watu
 
Shaka ni kiongozi na anafanya kazi kubwa Sana najua kila mwanachama anafahamu
 
CCM ni kielelezo sahihi cha ujinga wa watanzania.
 
Mwenzake aliyemtangulia alipita kwa 100% yeye kapita kwa 99% tu?!
 
Yeah....CCM ikae kitako, ipitie ajenda za wapinzani, izimeze zote na kuzitekeleza, watabaki holaaa, kiundwr kikosi Cha wataalamu wazichambue tu
 
Yeah....CCM ikae kitako, ipitie ajenda za wapinzani, izimeze zote na kuzitekeleza, watabaki holaaa, kiundwr kikosi Cha wataalamu wazichambue tu
Hii sahihi kabisa nakubaliana
 
Jangili mkuu wa Tembo wetu na ndio mwenyekiti wa CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…