Shaka Hamdu Shaka ziara yako HESLB ni mashaka matupu, mamlaka za juu zikusaidie

Shaka Hamdu Shaka ziara yako HESLB ni mashaka matupu, mamlaka za juu zikusaidie

Afrikasana

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2021
Posts
320
Reaction score
288
Ikumbukwe kwamba hivi karibuni katibu wa CCM itikadi na uenezi ndugu Shaka alienda bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu(HESLB) akitaka kujua ukweli wa mambo juu ya wahitaji kutopata mikopo hivyo malalamiko kuzidi kua mengi.

Baadhi ya wahitaji wamefika ofisi za bodi lakini watumishi hawawajali kabisa yatima na maskini ambao wanakila aina ya uthibitisho.

Watumishi wanatoa majibu mabovu kama vile hela hizo nizao na wanawapa wanaowataka.

Ukweli nikwamba watumishi wa bodi hawana utu na hawataki viongozi wao wajuu wafikiwe.
Wawakilishi wa kanda kwenye bodi za mikopo nao baadhi wanajiona ni miungu watu.

Wapo wazee ambao niwatumishi wa umma wanapewa mikopo,wapo wanaotoka familia bora na wanamiliki magari lakini wanamikopo ila wapo wanaotoka kaya maskini,yatima nk wameomba mikopo na rufaa wanakata lakini hawawajali kabisa. HESLB kuna shida kubwa isipotazamwa kwa jicho la tatu wahitaji wataacha vyuo maana hawana mbadala

Ukweli nikwamba wahusika wameshindwa kutenda haki na hata fomu wanazojaza waombaji hazipitiwi kwa kina bali nadhani kuna wakati wanacheza ana ana dooo maana yake mwenye bahati atabahatisha na kinyume chake pia sawa

Kutatua changamoto hizi,lazima wawajibishwe wahusika wakiwemo
Waziri wa elimu, Mkurugenzi wa bodi hiyo na menejimenti yote. Waziri na katibu husika hawajaguswa kabisa na hii kero kama vile haiwahusu.

Mh.Shaka unayo nafasi ya kumshauri Mh.Rais aitazame upya HESLB nawengine wanaozembea.
 
Kwa jinsi deni lake linavyonitesa kulipa. Simshauri hata kidogo kwa mtu mwenye uwezo angalau kuomba huu mkopo ni bora upambane na Ada otherwise kweli wewe ni mhitaji
 
Kwa jinsi deni lake linavyonitesa kulipa. Simshauri hata kidogo kwa mtu mwenye uwezo angalau kuomba huu mkopo ni bora upambane na Ada otherwise kweli wewe ni mhitaji
Wapo wahitaji hawapewi wanawapa ndugu zao wakaendeshe kampuni zao ambao hawatarejesha mikopo. Wakichunguzwa hao niwalarushwa wakubwa au watakua wanaongozwa na hisia kuliko uhalisia.
Watu tumefika bodi mwenzetu alilia na alizimia pale lakini hawakumpa mkopo wakati amepoteza wazazi wore. Hii nchi inawatu wanadhambi sana
 
Bila shaka ameenda kuuliza kwann vijana wake wa UVCCM hawajawekewa bumu.
 
Back
Top Bottom