SIMBA NYANI
Member
- Dec 8, 2014
- 35
- 25
JUMUI YA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) Zanzibar, imesema Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar,Maalim Seif Sharrif Hamad hana ubavu wala jeuri ya kuuyumbisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibara kuikwamisha Katiba Pendekezwa, anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka aliyasema hayo Zanzibar jana katika mkutano wake na waandishi wahabari akimtaka Maalim Seif asihadaike na uamuzi waserikali ya CCM kukubali kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK).
Alisema kuundwa kwa Serikali hiyo sio chochoro unaoweza kumfanya aingie Ikulu ya Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu ujao na hana ubavu,jeuri yakuizuia Katiba inayo pendekezwa isivuke bahari ili kufika Unguja na Pemba .
Mpango wake wakuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulio asisiwa na hayati Mzee Karume kwa, Tanzania haiwezi kufanya kituko chakuvunja Muungano wake wa miaka 50.
Katiba inayopendekezwa itavuka Chumbe, Bawe hadi Mtambwe naTaifa litabaki moja. ..Katiba Pendekezwa imeondoa kero na malalamiko yaliyokuwepo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ;hivyo hakuna Mzanzibari anayeweza kumsikiliza Maalim Seif ambaye amefilisika kisiasa,kiupeo na maarifa,alisema Shaka.
Aliongeza kuwa; Zanzibar imepata ilicho kipigania kwa miaka mingi,Rais wake ni Makamu wa pili wa Rais, mafuta na gesi asilia yameondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, hivyo Zanzibar itapata mikopo, kujiunga na tasisi za kimataifa bila kuvutwa shati au mtu mwingine kuizuia ,alisema. Shaka alisema UVCCM na Wazanzibari wanamjua Maalim Seif anachokitafuta ni kuiingiza nchi katika mifarakano na ikibidi watu wa mwage damu, kupoteza maisha nakupata vilema vya maisha.
Aliwaasa wananchi na kuwataka wayapime,wachuje nakutafakari maneno ya mwanasiasa huyo ambaye kila siku amekuwa mahiri na hodari wa kubadili ajenda za kisiasa kwa manufaa binafsi akiwatosa wenzake ndani ya CUF.
Tunamkumbuka alivyotembea nusu ya ulimwengu ili Zinyimwe misaada, chanjo za watoto wachanga na kinga kwa wajawazito;kwa hiyo kwa hili la Katiba amekwama na hawezi kulizuia,alisema.
Alisema kutokana na matamshi ya Maalim Seif kupinga Katiba inayopendekezwa, inathibitisha kuwa kiongozi huyo ni adui mmoja wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Akizungumzia uvumi wa aliyekuwa Mwana sheria Mkuu wa Zanzibar ,Othman Masoud Othman kuwa na mpango wakujiunga na CUF,Shaka aliufananisha na ganda la maua la jana ambalo mdudu chungu huo na kivuno wakati halina utamu.
CCM na Serikali zake hazina hofu na Othman,anaweza kwenda kuungana na Maalim Seif, Mansoor na Moyo ,CCM itakatambuga, haitayumba wala kutikisika, alisema.
Akihutubia mkutano wahadhara wa CUF mapema wiki hii, Maalim Seif ali iponda Katiba inayopendekezwa na kuwataka Rais Jakaya Kikwete na Dkt. Ali Mohamed Shein, kukata au shawishiwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi,Andrew Chenge akisema katiba hiyo haijapata ridhaa walau halali wa upande wapili wa Muungano.
Maalim Seif aliitaja Katiba inayopende kezwa kuwa haikupata theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar, hivyo haina uhalali wa kikatiba na kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano:scared: