Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,375
- 6,958
Ni kweli jamani mbolea ipelekwe kwenye mashamba yasiyokuwa na rutuba ili nayo pia yaweze 'kutoa mazao bora'.
Utakuta mtu anauwezo mkubwa kifedha anaoa au anaolewa na mtu mwenye uwezo pia, kwanini watu wenye uwezo wasioe au kuolewa na watu wasiokuwa na uwezo ili angalao tupunguze umasikini katika jamii zetu?
Angalia mifano;
Mume mbunge mke mbunge
Mume spika mama waziri
Mama ana degree tatu mme anazo tatu
N.k...
Tena wako warembo wa nguvu ila hawajasoma kabisa ila wako safi tu na maadili yao yako juu! Pia mijibaba iliyo kwenda angani lakini iko hoi kimaisha!
Jamani mnionaje hii....ni sawa kuliongezea mbolea shamba lenye rutuba?
Ndugu ume simplify sana.Nikuulize maswali machache:
Mazingira ya kukutana wapendanao, kitu cha kuwavuta pamoja je?
Kwani hao uliowaorodhesha walikuwa hivyo toka wanakutana?
Kupendana hakuangalii vigezo unavyotaka wewe - kuna wenye kupendana kwa sababu, kuna wale wanaopendana kwa sababu wanapendana n.k.Hakuna kanuni maalum.
Inategemea mlikutana kwenye mazingira gani na asili ya mtu.
Lakini kuna wanaume wengi wasomi na wenye uwezo wameoa wasichana wasiosoma na wasiokuwa na chochote anapoanza kukaa naye ndo anamuendeleza,
elimu ni kigezo, lakini sidhani kama ni kigezo muhimu sana wakati wa kuchagua mke au mume, kuna watu hawajasoma wana biashara zao nzuri wanazimanage na wana akili zingine za maisha na wametulia. inategea mtu unataka nini, kama huna majivuno au sifa ( nachukia wanaume wenye sifa sana) au kutaka watu wakuone
Na wanaume wabinafsi anaona akioa mtoto wa maskini atamtegea kwa kila kitu na yeye ana umimi anataka kila kitu chake kiwe chake mwenyewe badala afikirie nitamuendelezaje na yeye aweze kusimama kwa miguu yake.
Wewe "mkali" sana sister nimekukubali, ila hii kauli imenisisimua kweli!! na nadhani sijaelewa kwanini uwachukie kiasi hicho, ndivyo walivyo tu dada!
sikiliza nikuambie kaka yangu, mwanaume mwenye sifa na majivuno ni lazima atakudharau tu hata iweje. hata ukifanya zuri au ukijitahidi sababu yeye ameshazoe kujiupgrade anakuona wewe siyo kitu kabisa, kazi ni kukuvunja moyo.halafu mwanaume mwenye sifa hajifichi siku ya kwanza tu utajua.