Shamba linauzwa

Shamba linauzwa

Maxence Melo

JF Founder
JF Staff
Joined
Feb 10, 2006
Posts
4,324
Reaction score
13,967
Lipo maeneo ya: Vianzi/Vikindu

Lina ukubwa wa hekari 20,

Lina hati ya serikali ya kijiji ya umiliki.

Umbali: Kilomita 35 kutoka mnara wa saa (Clock Tower) Mnazi mmoja hadi hapo shambani

Gari ndogo linafika hadi shambani.

Bei Tshs Milioni 20.

Kwa mawasiliano nitafute nikuunganishe na muuzaji (si dalali) mwenyewe. Simu yangu +255713444649 au barua pepe
Code:
maxence@maxence.co.tz

Shamba likishauzwa mtafahamishwa ili mjadala ufungwe.
 
Lina mazao gani au ni pori ambalo ni virgin, tuambie na hali ya ardhi kama mimea inastawi na aina gani,lipo flat, bondeni, kuna mto karibu nk
 
Mkuu mi naweza nikatafuta mteja na nikamleta?
Lakini kifuta jasho si kipo au?
 
Lina mazao gani au ni pori ambalo ni virgin, tuambie na hali ya ardhi kama mimea inastawi na aina gani,lipo flat, bondeni, kuna mto karibu nk
Well,

Baada ya kuongea na uncle, amenifahamisha kuwa shamba liko flat (lakini si kama meza) na mimea ya aina nyingi inayostawi Pwani inastawi vema na majirani zake wamelima mazao ya msimu pamoja na michungwa. Pia pembeni mwishoni mwa shamba kuna bonde ambalo lina mto ambao ni wa msimu lakini ni mara chache kukauka.

Limefyekwa karibia robo yake lakini eneo lililobakia lina vichaka vidogo vidogo ambavyo vinapitika.

Mkuu mi naweza nikatafuta mteja na nikamleta?
Lakini kifuta jasho si kipo au?
Kamisheni? Sawa, tutaongea mkuu maana nami ni mjumbe, lakini kwako si neno, inaongeleka.
 
Lipo maeneo ya: Vianzi/Vikindu

Lina ukubwa wa hekari 20,

Lina hati ya serikali ya kijiji ya umiliki.

Umbali: Kilomita 35 kutoka mnara wa saa (Clock Tower) Mnazi mmoja hadi hapo shambani

Gari ndogo linafika hadi shambani.

Bei Tshs Milioni 20.

Kwa mawasiliano nitafute nikuunganishe na muuzaji (si dalali) mwenyewe. Simu yangu +255713444649 au barua pepe
Code:
maxence@maxence.co.tz

Shamba likishauzwa mtafahamishwa ili mjadala ufungwe.

Nashukuru Mkuu, ila sasa Vianzi ama mbele ya Vianzi maana isije ikawa mbele kule kwenye mashamba ya Mahita he he he
 
Mkuu tupe maelezo ya shamba lenyewe tukianzia na kama lina mazao, aina ya udongo, huduma za jamii zilizopo. n.k. Nikishapata details za kutosha nitawasiliana na wewe. Otherwise, thanks kwani unapenda maendeleo.
 
Nashukuru Mkuu, ila sasa Vianzi ama mbele ya Vianzi maana isije ikawa mbele kule kwenye mashamba ya Mahita he he he
Ni hivi,

Nimeongea na uncle anasema shamba lipo mbali kidogo na kwa Mahita. Kama unaenda na daladala unashuka kituo kinaitwa Majumba Sita na ukienda kwa gari binafsi ukifika Majumba Sita kuna njia ambayo inakupeleka moja kwa moja mpaka shambani.

Mkuu tupe maelezo ya shamba lenyewe tukianzia na kama lina mazao, aina ya udongo, huduma za jamii zilizopo. n.k. Nikishapata details za kutosha nitawasiliana na wewe. Otherwise, thanks kwani unapenda maendeleo.
Mkuu Maane,

Shamba kwakuwa ni kubwa lina maeneo ambayo yana maji kiasi unaweza kupanda mpunga na kuna eneo ambalo lina mchanga (wa wastani si mwingi) ambalo hata mvua iwe nyingi kiasi gani hapawezi kutota kwa maji (manake hata kujenga nyumba unaweza).

Ahsante... Maswali zaidi?
 
Je bei ni ya mwisho hakuna maongezi? Anapatikana lini twende kuliona?
 
Liko karibu na Kijiji cha Kisemvule ama karibu na ilipokuwa `Polo Italia Amadori` au karibu na ilipokuwa `stop over bar`?, kuna maelewamo ama bei haishuki?
 
Kama nikitaka robo ya eneo lote (hekari 5), inawezekana?
 
Je bei ni ya mwisho hakuna maongezi? Anapatikana lini twende kuliona?
Anapatikana kuanzia kesho kwa maongezi na kuliona Shamba nadhani itapendeza kuwa kuanzia Ijumaa. As long as uko tayari jamaa yangu yupo tayari pia kukupeleka mpaka eneo lenyewe.

Liko karibu na Kijiji cha Kisemvule ama karibu na ilipokuwa `Polo Italia Amadori` au karibu na ilipokuwa `stop over bar`?, kuna maelewamo ama bei haishuki?
Kabla ya kufika Kisemvule. Ni mpaka maeneo ya Majumba Sita baada ya kuvuka kwa Mahita.

Ni mtanzania na hivyo maelewano yapo tu.

Samahani wakuu...hivi Vikindu ni kuelekea kule Mbagala mbele?
Ndiyo mkuu Yebo Yebo, ni maeneo ya mbele baada ya kuvuka Mbagala barabara ya Kilwa.

Maswali zaidi????
 
Huu mchongo ngoja niuhangaikie unaweza ukatoka kwenye game hivi hivi kwa kula %.
 
Nashukuru Mkuu, ila sasa Vianzi ama mbele ya Vianzi maana isije ikawa mbele kule kwenye mashamba ya Mahita he he he

Mbona mashamba ya Mahita yapo pale Vianzi njiani kabisa? lile la barabarani amejenga na banda, la mbele yake kama unaenda Marogoro amepanda, michungwa, migomba etc.....hili la Max liko mbele kidogo!

Wakuu kule kuna ardhi yenye rutuba sana, usafiri wa daladala upo....mazao yanayostawi ni kama migomba, mpunga, mahindi, maharage,mihogo, michungwa, nanasi, pensheni, watermeloni etc!

Kama mtu yupo serious anahitaji ardhi, huko ni mahala pake!

Duh Mkuu Max huko, kuna kijishamba changu pia sijaenda muda mrefu sana kisije unganishwa...(joke)!
 
kuna shamba pia lipo maeneo ya changanyikeni. lina hati miliki ya wizara. ni zuri lina ukubwa wa ekari tatu kasoro. (prime area)
bei ya kuanzia 200 milion (siriaz).
pia kupangisha ni plan B
kama kuna buyer makini wasiliana na Max atanistua.
 
Duuu mkuu mzee MAXMELO yeye anataka kwa eka 20 milion 20 sasa wewe eka 3 kasoro milioni 200 sasa wapi na waspi??Na umefanya hivyo kwa ajili ya umbali au inakuwaje hapo?
 
I see hilo shamba la heka 20 mhusika anakubali kulipwa mara nne kila mwezi robo ya bei?
 
Back
Top Bottom