Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

Pasco nakuuliza uwe mkweli ktk nafsi yako!! Hivi hizi hotuba mbili za bwana mkubwa una act kuzisahau?!
1. Hotuba ya siku ya makinikia ya omera mwenzangu!! "Huwezi kuwa msaliti uka survive"
2. Na ile prof. Mruma spika alipopongezwa na kuagizwa "Hongera kwa kuwadhibiti bungeni endelea hivyo ili waje waropokee huku nje nami nitadeal nao na siwatishi"

Najuwa watu wanafanya juhudi ya kupotezea lakini watu kama kina Mobutu hawakutumia mikono yao bali makundi yaliyoandaliwa na kulelewa. Kumbuka Premio ya blue na Nissan nyeupe lakini waliomo hawajulikani [emoji40] [emoji40] [emoji85] [emoji120] [emoji120]
 
Mkuu paskalis,ili kupunguza na kuondoa kabisa hizi conspiracy theories kwanini hii gvt isilete Scotland yard or FBI?we need answers and we need them quickly
Kwa kutambua kuwa nae ni mtuhumiwa CDM amekubali ufanyike uchunguzi huru,mtuhumiwa mwingine GOT yuko kimya hajakubali wala kukataa hadharani uchunguzi huru nafikiri anapima upepo ili aamue la kufanya,mtuhumiwa wa tatu CCM yeye nadhani kachanganyikiwa hajui la kufanya ila wapambe wake humu mtanfaoni wanadai kukubali uchunguzi huru ni kujidharirisha kwani nchi inao wapelelezi wa kutosha, ni kweli ila inategemea na utashi wao ndio maana mzee wa bastola hajulikani ingawaje wanamjua.
CDM kauvua mzigo kawaachia wenzie kuchagua wakubari kubeba lawama ama watoe kafara wawakamate wahusika ama wakubari uchunguzi huru, la sivyo jina la hitmans linawahusu.
 
Pascal mayalla ..kwa huu uzi kama watu watakutukana wasamehe coz ni wajinga na ni washabiki wasioweza chimba jambo ,yote uliyosema ni ukweli ukitizama tukio lina ujanja ujanja mwingi tangia kwa dereva wa lisu,,,ukwelii huu uzi umeenda shule wajinga watakejeli ila mwenye akili timamu suala la lisu linaweza kuwa na watu walioshiriki ambao siku wakijulikana watu watashangaa ,,,,,niseme tu wanaishi nyumba moja na mbaya anaweza kuwa ndani yao ,,,hata yesu alisalitiwa na yuda mwanafunzi wake ,,,,ni suala la muda tu,,,uenyekiti kazi kweli aiutaki jaman cdm
 
Mafumbo kama kwenye Kanga!!!!!!
Pasco amekuwa pasi ya mkaa ya Magufuli siku hizi. Tangu anaanza andiko refu lenye marembo nilijua mwisho Wa siku atakuja kumtetea ndugu yake. Pasco unamdanganya nani kuhusu Lissu. Huyo ndiye threat halisi dhidi ya mjomba wako Magufuli na yeye anajua ndo maana kila siku haachi kumtaja kwenye mikutano hata kwa mafumbo. Pasco unazeeka vibaya, na vyeo vya kuteuliwa vimepunguwa labda wakupe Ukatibu Tarafa huko RUKWA.
 
Kakae jikoni umsaidie shemeji kukuna Nazi huna lolote mnafiki tu. Tukio la Lissu lingefanywa na wapinzani serikali ya ccm ingeshawaweka peupe mapema! Mnajifariji wakati mnatembea na damu mikononi.
 
Hoja zako haziekeweki kwa jinsi ya uandishi wako mbovu.
Kuwa tu muwazi, japo haueleweki ila.
Serikali inapenda sana kujiingiza kwenye kuchochea migogoro mfano ule wa CUF. Hilo unalichambuaje?
 
Kwa jinsi lilivyoelewa hili bandiko ni kwamba "wale jamaa" hawahusiki maana njia iliyotumika kwa LT sio njia ya "wale jamaa" (njia yao ni clean and soft)

Pili inside job inahusika kwa ℅kubwa.


Maoni yangu, may be ni "wale jamaa" ila wamedisguise kama amaturs na wame wamanipulate victim pati ile chochote kitakachotokea (God forbid) walaumiwe wao kwa ukaidi wao.

Ila sija eliminate inside job.

Pia napenda kujua, how well this thread is secure.
 
Umesomeka! Akili kubwa itang'amua dhima ya Uzi wako bila kutokwa na povu.
 
Mku nimemwelewa Pasco kidogo. Nilichomwelewa hapa amewachokoza wahusika ila chadema kuingiza kama kuchokoza mada vile yaani kama kwenye daladala ili mjadala uanze. Mku Muvi kaiweka wazi Sana yaani kaulizwa mtu hivi Je wale waliotajwa na yule Bloga wa Kenya mbona kimya na kimya wao unazaa jambo lenye ukakasi.
Mimi nimemwelewa hivyo
 
Kaka Pascal Mayalla , Mark Mwandosya yeye ilikuwa nini?, je yule Mwenzie aliyekuwa anababuka ngozi kama Nyoka, pamoja na hayo kulikuwa na mtu alikamatwa kwa kusema uongo kuwa Mwamunyange kapewa sumu
Hivi Mtikila ilikuwaje?
 
Muhusika wa shambulizi la Lissu ndiye huyo huyo mhusika Mkuu wa kutekwa na kupotea kwa Ben Saanane, na ndiye huyo huyo muhusika wa kutekwa kwa Roma. Huyu ndiye Mkuu wa kikosi cha watu wasiojulikana anayetoa go ahead ya nani wa kumteka, kumtesa na hata kumuua baada ya kupata ruhusa toka kwa baba yake. Kumbuka kauli yake ya Roma kupatikana kabla ya Jumapili na ikawa kweli.

Huyu ni muuaji ambaye alistahili kuwa jela siku nyingi sana. Kumbuka pia kauli ya kuwashughulikia wapinzani ndani na nje ya Bunge. Nje ya Bunge aliyepewa ruhusa ya kuwashughulikia wapinzani na wanaompinga huyu aliyejawa na chuki si mwingine bali ni huyu Mkuu wa kikosi cha watu wasiojulikana cha utekaji, utesaji na uuaji anayeitwa DAB.


 
nimewa kusikia hisi simulizi za mfumo wa vyama vingi kuwa ni maboya kwa mabepari Mzee aliruhusu kwa sharti la kupeleka watu 'wasiojulikana' kuanzisha hivyo vyama na kama ni kweli basi dhana ya watu kufariki kwa matukio tata au kupata ajali tata hasa nyakati za uchaguzi wa ndani inaweza kuwa nq mashiko endapo hawa wahanga sio miongoni mwao 'wasiojulikana'
 

Mkuu usipoteze lengo,Watanzania wote wanajua kuwa raisi wetu hataki kukoselewa,watanzania wote wanajua kuwa Tundu Lisu ndie mkosowaji mkubwa wa raisi....

Watanzania wanashuhudia vipi mawakili wanachomewa moto au kupigwa mabomu offisi zao....,labda uwe huna akili timamu ili usifahamu nini kinaendelea Tanzania hivi sasa..
 
Nadhani hawa wanawajua wasiojulikana kama TCRA ikiwatafuta na kuwauliza inawezekana wakawataja wasiojulikana
 

Attachments

  • TCRA2.jpg
    56.7 KB · Views: 85
  • TCRA.jpg
    31.1 KB · Views: 85
Usipate Shida kuzunguka mbali hii movie ya Sasa ilibuniwa na kuratibiwa na Maliyamungu Bashite wa Dsm mjukuu wa Maliyamungu wa enzi za idd Amin Dada , ambaye alikwenda Dodoma na alikuwa ndani ya Nissan nyeupe akitoa Amri, kwa kuwa si mzoefu wa Umafia alitoa Amri za kukurupuka kwa Uoga mwingi ndipo wapigaji Risasi wakapiga kwa haraka pasipo kulenga vizuri wala kushuka kuthibitisha kama lengo limetimia, oparation ilifabywa na mtu ambaye sio mzoefu ndiyo maana ilifeli kama mission zake nyingi ikiwemo ya Roma na clouds, Le mutuz Jerry muro na Lipumba wanajua A-Z ya Sinema zote wakiletwa FBI, Scotland Yard wakawahoji ndani ya Dk 20 tu watabaini Ukweli wote kwani tukio la Lisu lipo wazi ingawa vijana wa Le mutuz wapo busy saa 24 mitandaoni kutengeneza propaganda na Uzushi wa kuwatoa watanzania kwenye njia sahihi ni vigumu kuwabadili ni vyema pesa anazopewa le mutuz zitumike kujenga Hosptal kubwa ya kisasa Zanzibar na Dsm iwaajiri madaktari toka india, ulaya na marekani watanzania na Nchi jirani waje kutibiwa kuliko kupoteza mabilioni kuwalipa hao wajinga kutengeneza propaganda na mipango ya hovyo hovyo isiyo na Tija kwa Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…