Shambulizi kwenye kituo cha Ebola DRC laua wafanyakazi 4 na kujeruhi 5

Shambulizi kwenye kituo cha Ebola DRC laua wafanyakazi 4 na kujeruhi 5

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirika la afya duniani (WHO) limesema mashambulizi mawili yaliyotokea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yamesababisha vifo vya wafanyakazi wanne wanaoshughulikia mlipuko wa Ebola nchini humo na wengine watano wamejeruhiwa.

WHO imesema mashambulizi hayo yalitokea usiku kwenye kambi ya pamoja ya machimbo ya Biakato na ofisi ya uratibu wa ushughulikiaji wa Ebola huko Mangina, mji mdogo katika jimbo la Kivu Kaskazini. Watu waliouawa ni pamoja na mhudumu wa kikundi cha chanjo, madereva wawili na ofisa wa polisi.

Mkurugenzi wa WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, ugonjwa wa Ebola unaondoka, lakini mashambulizi hayo yanaupa nguvu ugonjwa huo tena, na matokeo yake ni kuwa watu wengi zaidi watakufa. Amemtaka kila mtu atoe mchango na kukomesha mzunguko huu wa vurugu.
 
Dah..hao watu sijui wasaidiwaje..maana Ni vichwa ngumu balaa
 
Back
Top Bottom