Shameful!

semenya, hizi ndoto za vyama vya upinzani kujipanga zimeanza leo? jamani, kuna nyakati tujikumbushe kuwa... unless the grain of wheat dies...
Mkuu what should we do? Vita? me sioni kama vita ni solution, wapi pametengemaa after vita? Iraq, Afkhanstan? utaniambia Rwanda, ila cunaona Kagame ni dikteta na panaweza pakatokea vitangine pale. So kwa hapo naonyesha jinsi gani vita ilivyokua mbaya na si solution kaka, hii JF utakua hauipati mkuu tukizipiga hapa.
 
lakini sasa mbona hii njia mbadala nayo hainyeshi nuru yoyote? unajua, next year, uchaguzi unakuja, mijamaa inaiba kura, miafrika ndivyo tulivyo, wengine wanawapa kura... jamaa wana claim mandate ya kufanya utumbo wao, sisi tunabaki kulalama hapa jf. mpaka lini wandugu?
 
Wasipowapigia kura CCM!!!wawapigie nani???Lazima tukumbuke kwamba jini likujualo halikuli likakwisha......upinzani wenyewe hovyooo hao ndo wataimaliza kabisa nchi bora chama cha mafisadi kiendelee........ndo hio.
 
inauma sana aisee. and there is another 5 years for us to take the same shits.
 

Well said, wa-TZ wana utamaduni wa kulaumu kila mtu isipokuwa wenyewe.

Wa-TZ wajilaumu wenyewe kwa kubariki uongozi bomu.

Well said!!!
 
Believe me; hatuwezi kuwalaumu wananchi moja kwa moja. Wananchi wanahitaji kuoneshwa uongozi, sasa hivi uongozi huo haupo na tumekuwa kama ng'ombe walioachwa nyikani wakitarajiwa wajirejeshe zizini huku chui wanawanyatia!
 
Mimi naona serikali ya Chama Cha Majambazi imefanya makusudi kuhakikisha kwamba barabara za kwenda mikoani mpaka vijijini ni mbovu na zisitengenezwe kwasababu....zikiwa nzuri, habari zitawafikia wananchi kiurahisi na watafumbuliwa macho.
Ili "Ufisadi" uendelee kushamiri, hili jambo lilitiliwa mkazo sana. Nasema haya kwasababu....

Kwanini sisi tu ndio tuwe na mabaranara mabovu yasiyopitika mpaka leo? Kwa mfano: Kenya wametandika lami mpaka lake Turkana. ...

Pia kwa vile sisi waTanzania tumezoea kukaa kimya katika mambo mengi yasiyotupendeza, yanayofanywa na serikali, basi na serikali nayo inaonatuona kama "ma-mbumbumbu" yasiyoweza kuuliza chochote kile...na "ufisadi" unaendelea.

Ukifika wakati wa uchaguzi....vijisenti vinatembezwa kwa viongozi wachache...midundiko inapigwa hapa na pale...watu wanakunywa Bia za bure (kutoka kwenye pesa za wizi CCM)...halafu CCM inarudishwa madarakani.

Kwa hiyo....mpaka wananchi wapatwe na mwamko na kuitoa CCM madarakani, na viongozi wote wa CCM waondolewe, na Serikali yote ibadilishwe....labda uchumi maisha ya wananchi vitabadilika.

My Opinion.
 

Dr Kitila,

Do we really have alternative party?. BE HONEST
 
This country needs a leader like Putin who can deal with hawa mafisadi the same way Putin dealt with the oligarchs....
 
Wasipowapigia kura CCM!!!wawapigie nani???Lazima tukumbuke kwamba jini likujualo halikuli likakwisha......upinzani wenyewe hovyooo hao ndo wataimaliza kabisa nchi bora chama cha mafisadi kiendelee........ndo hio.


mmh, mimi naona jini ccm ni tofauti. maana linakula kila kitu
mithili ya mfalme jeta. na linakula na kukwisha!!
 

Si amtie EL na washirika wake Lupango tu! Yeye ni mkulu wa nchi anaweza kutumia sababu lukuki.
 

Kikwete hana tatizo, Wabunge hawana tatizo, CCM hawana tataizo. Tatizo liko kwa watanzania wenyewe maana huu ndio utawala wanaoupenda kutokana na ukweli kuwa asilimia kubwa ya watanzania wamedumaa kiakili.

Hivi inmawezekanaje watanzania wanaona wazi kuwa hawana viongozi ila wahuni tu wanaotupiana matusi na bado wanakaa kimya bila kuandamana na kutaka uitishwe uchaguzi mkuu wachaguliwe viongozi waadilifu? Maana imeonekana wazi kuwa hakuna kiongozi muadlifu kwenye CCM. Wabunge wote wezi, mawaziri wote wezi, Spika mwizi.

Ni kiongozi wa muhimili mmoja tu yaani Chief Justice ndio muadilifu. Basi aachiwe yeye aunde serikali ya mpito maana mpaka sasa ni chaos tupu.
 
Ni aibu kwa wabunge wanaojiita wapambanaji wa ufisadi nao kujikuta wamenaswa na mtego wa ufisadi kumbe nao ni maafisadi ila walikuwa hajapata nafasi hiyo ndiyo sababu wanapige kelele ya ufisaidi.Sasa baada ya kunaswa wanataka kuhalalisha ufisadi wa kuchukuwa posho mara mbili kwa kazi moja kuwa ni halali.Hongera Mkurugenzi wa Takukuru EH timiza wajibu wako na hao maafisadi wasikutishe.Wanatafuta umarufu tu na kujisifu kumbe ni maafida wakubwa
 
Ni aibu kwa wabunge wanaojiita wapambanaji wa ufisadi nao kujikuta wamenaswa na mtego wa ufisadi kumbe nao ni maafisadi ila walikuwa hawajapata nafasi hiyo ndiyo sababu wanapiga kelele ya ufisaidi.Sasa baada ya kunaswa wanataka kuhalalisha ufisadi wa kuchukuwa posho mara mbili kwa kazi moja kuwa ni halali.Hongera Mkurugenzi wa Takukuru EH timiza wajibu wako na hao maafisadi wasikutishe.Wanatafuta umarufu tu na kujisifu kumbe ni maafida wakubwa
 

Ingawa Bunge limeamua kutulia kuhusu sakata la Richmond, lakini taarifa zilizopo ni kuwa, kuhojiwa kwa wabunge na Takukuru bado kunaendelea.. Sijui taarifa hizi ni sahihi? Mwenye undani zaidi pse advise..
 
Nina kiri kwa moyo wangu na kutamka kwa Ulimi wangu ni KWELI CCM TUNATATIZO KUBWA tumeahidi kwa muda mrefu hatujatekeleza ninajuta kuwa nami nisehemu inayowatendea watanzania maovu haya kwa imani yangu ninafahamu Mbele ya macho ya watanzania na mbele ya Mungu Tunamakosa.

Kwa kipindi cha miaka mitatu nimekuwa nikijiuliza nini suluhisho sijapata hata huko ktk Upinzani nina amini kuwa hawataweza kutatua matatizo haya

Kubwa linalo niumiza ni kuwa toka mwaka 2006 taifa hili limepitia SINEMA za KUIGIZA Nyingi sana kuanzia
SINEMA YA BOSI WETU KUPITIA WIZARA MOJA MOJA KUWAPA VISSION YAKE,
SINEMA YA UKAME
SINEMA YA RICHMOND
SINEMA YA BUZWAGI
SINEMA YA KAMATI YA MADINI
SINEMA YA EPA
SINEMA YA MRAMBA NA YONA
SINEMA YA KIWIRA
SINEMA YA KAMATI YA MWAKIEMBE
SINEMA YA POSHO MBILI
SINEMA YA KIWIRA
SINEMA YA WAPAMBANAJI WA UFISADI
SINEMA YA SPEED AND STANDARD
SINEMA YA KAMATI YA MWINYI
SINEMA YA KILIMO KWANZA
SINEMA YA MAFISADI PAPA NA NYANGUMI

Hizo ni baadhi ya sinema ambazo kwakweli zimekuwa zikiniumiza najua sisi tunaoishi huku mwisho wa Nchii hii tunaona umasikini ulivo,kuna umasikini wa hali ya juu ninafahamu na kukiri kabisa kuwa miaka hii mitano taifa limebaki ktk midahalo isiyokuwa na mantiki na sisi wanachi na vyombo vya habari tunashirki kwa kiwango kikubwa kuifikisha nchii hii ktk hali ya leo,sina uongozi CCM bali ni mwana CCM nafahamu tumetenda dhambi kubwa tutatokaje mpaka sasa sina majibu
 
Mwanakijiji,

The whole threat was oky but this one i dont thinks u whre right to depict this way

"Shame on all you CCM members who have tolerated and excused this level of stupidity disguised as democracy in the party!"


To my opinion it should be

"Shame on all you NEC-CCM members who have tolerated and excused this level of stupidity disguised as democracy in the party!"

Kwa sababu NEC ndio huenda pale DODOMA na kututengenezea makundi na kumpitisha mgombea bomu na kutufanya wana CCM wengi hamunazo its really painful
 
M-Bongo

Kubwa linalo niumiza ni kuwa toka mwaka 2006 taifa hili limepitia SINEMA za KUIGIZA Nyingi sana kuanzia
SINEMA YA BOSI WETU KUPITIA WIZARA MOJA MOJA KUWAPA VISSION YAKE,
SINEMA YA UKAME
SINEMA YA RICHMOND
SINEMA YA BUZWAGI
SINEMA YA KAMATI YA MADINI
SINEMA YA EPA
SINEMA YA MRAMBA NA YONA
SINEMA YA KIWIRA
SINEMA YA KAMATI YA MWAKIEMBE
SINEMA YA POSHO MBILI
SINEMA YA KIWIRA
SINEMA YA WAPAMBANAJI WA UFISADI
SINEMA YA SPEED AND STANDARD
SINEMA YA KAMATI YA MWINYI
SINEMA YA KILIMO KWANZA
SINEMA YA MAFISADI PAPA NA NYANGUMI
SINEMA YA HALI MPYA,NGUVU MPYA NA KASI MPYA
SINEMA YA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA
SINEMA YA KAULI TATA ZA VIONGOZI NA AHADI ZISIZO TIMILIKA
SINEMA YA KUPOTEZA KABISA KUTAMBUA ALAMA ZA NYAKATI
SINEMA YA NEC KUWA WABISHA NA KUTOKUKUBALI KUWA KUNA MAPUNGUFU TENA MAKUBWA NDANI YA CCM YETU
 
Shame on each one of us who end up shouting and barking at the wrong tree. Most of us never serious with our own lives let alone our own intentions. We been made to believe that hard work never pays and in fact our own government has made sure that any hard working Tanzanian does not make it unless they go through the prescribed channels. Believe me I can list hundreds of intellectuals who are have been frastruated by this government. Wewe nchi hii kwa sasa bila connection ya mzito au kada wa CMM hufiki popote. Ukiwa unajuana na Tanil au Rostam au Jeetu na kwa wengine Mengi na Membe, it is even more easier. Sisi binafsi tumelikubali hilo rasmi na tunapigana vikumbo tukigombania kutambulika na hao waliowahi! Sasa leo wanvuana nguo tunalia aibu; aibu gani kwani tulitegemea lipi?

Lingine la kusikitisha ni kwamba sisi wenyewe tuna biases zetu kiasi ambacho hata kama unauona ukweli unaukataa katakata kwa sababu flismy; Kwa mfano kuwa wengi wetu tunaoshabikia "ufisadi" wa Lowassa na ukiulizia tuna ushahidi gani ambao unaweza ukachujwa katika misingi ya uwazi with open minds, utaambiwa Ripoti ya Mwakyembe inaeleza wazi, wakati Mwakyembe mwenyewe anakiri kuwa ana ushahidi ambao hakuutoa kwa makusudi ili kutokuiaibisha serikali na kwa maneno hayo tunakubaliana naye. Hivi does it make sense?

Tumeshalemazwa na maneno matupu in the names of "ufisadi" "upiganaji against ufisadi" na tumekuwa tunafuata upepo tu bila kuwa na misimamo yetu binafsi, na sasa baada ya kuona hao tunaowaabudu na kuwasikiliza bila ya analysis yoyote wanaanza kuvuana nguo hadharani ndio tunaanza kupiga mayowe "aibu aibu aibu"! Shame on us in the first place tunayashabikia mengi ya uwongo na uzushi hata kama ukweli unaoonekana wazi to the contrary.

Kwa mfano swala la Richmond ambayo kamati ya Shelukindo iliwakilisha ripoti ya rasmi ya utekelezaji wa serikali wa maazimio ya kamati bungeni August mwaka huu na bunge ikaikubali ripoti hiyo pamoja na mapungufu ambayo serikali iliombwa iyafafanue zaidi kuhusu utekelezaji wake. Sasa unakuta kuwa badala ya kuzungumzia maazimio yale ambayo serikali iliombwa iyafafanue zaidi kuhusu utekelezaji wake, unakuta tunazungumzia ripoti yote kwa ujumla wakati kuna maazimio kibao zaidi ya 18 ambayo utekelezaji wake ulikubaliwa na kamati; kwa mfano azimio #14 na 20 kuhusu kuwajibishwa kwa waliohusika na kuwepo kwa rushwa kwenye mchakato, maazimio ambayo utekelezaji wa serikali ulikubaliwa na kamati kwa niaba ya bunge. Lakini bado hata sasa hivi tuko wengi ambao hatujaridhika na utelezaji wake ingawa kamati yeneyewe imeandika rasmi kuridhika na hayo. Haturidhiki kwa vile tayari tuna misimamo yetu ambayo bila kuridhishwa basi tutapiga kelele, hala tunashangaa kuona wale tunaowashabikia kuvuana nguo hadharani. Wote tuko sawa tu wala tusijidai wanatuaibisha.

Ni hapo ambapo tutaamuwa kuwa objective kwenye mazungumzo yetu hata kama linalosemwa linatukera, pale ambapo ukweli tutaukubali kwa gharama yoyote ile, pale ambapo hatutamkubali mtu tu kwa ajili ya jina lake an sura yake au kwa pesa zake, then viongozi wetu itabidi waamke na kujua kuwa wameshagunduliwa janja yao. Mtu kama Sitta na scandals zake za CDA, TIC anadiriki kusema kuwa wanaopinga 2xPOSHO wanawaonea wivu wabunge. Kweli hiyo ni statement ya Spika wa bunge. Mbona spika wa uingereza aliachia ngazi kwa issue ya 2xAllowances. Halafu na sisi tunashabikia wazi kuwa kuchukua posho zaid ya mara moja ni sawa ukilinganisha na Richmond. Kwani unadhani anayechukua posho mara mbili akipata mwanya wa Richmond atauachia?

So long as mafisadi "dagaa" na "mafisadi" papa watakuwa na washabiki na wafuasi ambao wanawasikiliza bila kuwahoji tutakuwa tunaipeleka kesi ya nyani kwa tumbili, na itakuwa issue ya nyani kutukuliona kundule!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…