Shamira Mshangama Akabidhi Simu 9 na Kadi 1,000 za UVCCM Mkoa wa Tanga

Shamira Mshangama Akabidhi Simu 9 na Kadi 1,000 za UVCCM Mkoa wa Tanga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SHAMIRA AKABIDHI SIMU 9 NA KADI 1000 ZA UVCCM TANGA.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) viti vitatu Bara Shamira Mshangama amekabidhi Simu Tisa, pamoja na kadi za Uanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) 1000, Kwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ramadhan Omary ili kufanikisha usajili wa wananchama ndani ya mkoa wa Tanga

Akizungumza kwenye Baraza la Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Shamira amesema lengo la kutoa Simu hizo ni kuongeza kasi ya Usajili wa wananchama wapya kwa njia ya Kielektroniki katika mkoa huo pamoja na kutunza Taarifa za usajili.

“Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ostadh Rajab Abdulrahman ana nia ya dhati ya Tanga kuongoza kwa kura kwenye chaguzi zote Tanzania. Hivyo sisi vijana wake lazima tuhakikishe tunaongeza idadi kubwa ya wana CCM na wapiga kura”.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga Ramadhan Omary amesema simu hizo zilizotolewa zitakwenda kusajili wanachama Kielektroniki kama ilivyokusudiwa ambapo kwasasa kasi ya usajili itaongezeka katika kupata wanachama wapya.

WhatsApp Image 2024-09-05 at 11.35.14.jpeg
WhatsApp Image 2024-09-05 at 11.35.14(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-09-05 at 11.35.15.jpeg
WhatsApp Image 2024-09-05 at 11.35.15(1).jpeg
 
Back
Top Bottom