Pre GE2025 Shamira Mshangama: Vijana lazima tuyaseme makubwa yanayofanywa na Dkt. Samia

Pre GE2025 Shamira Mshangama: Vijana lazima tuyaseme makubwa yanayofanywa na Dkt. Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Tanzania Bara Ndg. Shamira Mshangama akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Vijana CCM na kuhamasisha ushiriki wa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.

1739974107617.png
Shamira Mshangama katika ziara yake ya Mkoani Simiyu amechangia pesa kwa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Simiyu inayoongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Elias Nyasilu, kwa ajili ya kusapoti ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM mkoa wa Simiyu, pia alichangia ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Bariadi kwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bariadi Ndg. Tinana Masanja

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesisitiza kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake.

"Naamini nyumba hii ya Katibu wa UVCCM ikikamilika itaenda kupunguza baadhi ya gharama ambazo Jumuiya inaingia katika kumtafutia sehemu ya kuweka malazi Mtendaji wetu wa vijana."
1739974168068.png
Mwisho, Shamira alipata wasaa wa kuzungumza na viongozi pamoja na wana CCM wa kata ya Nyangokolwa iliyopo katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kuwaasa juu ya kuendelea kuyasema mazuri anayoyafanya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye maeneo yote wanayotoka ili kuhakikisha ushindi wa kutosha kwa Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu 2025.

1739974198761.png
 
Nasikitika kusoma na huyu binti, alikuwa sijui vice president wachuo. Hewa kabisaa.
 
Back
Top Bottom