Shamsa Ford: Vijana wengi wa kiume wa Dar ni wambea, chawa na VibenTen.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


Msanii wa filamu Shamsa Ford amedai vijana wengi wa kiume wa Dar es salaam ni chawa, wambea na vibenten kwa kuwa walikosa elimu ambazo zingewawezesha kwenda kushindana kwenye soko la ajira.

Muigizaji huyo amedai wanaume anatakiwa kuwa na misimamo na muonekano wa kiheshima katika jamii na sio kuonekana wakifanya mambo ya ajabu.

“Wanawake wenzangu tujitahidi sana kuwapa elimu ya kutosha watoto wetu wote haswa watoto wa kiume. Nimejikuta kuwa na huruma zaidi na watoto wa kiume kwasababu wa kwangu ni wa kiume. Huwa naumia sana nikiona mtoto wa kiume anavyoangaika kupata riziki,” aliandika Shamsa Ford kupitia Instagram yake.

Aliongeza, “Mtoto wa kiume asipokuwa na elimu ya kutosha au ujuzi wowote mwisho wao huwa ni mbaya kuliko watoto wa kike. Sasa hivi vijana wengi ambao hawana kazi au hawakubahatika kusoma ndo WAMBEA,WAPAMBE,VIBENTEN MARA CHAWAAA,”

Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema atahakikisha kwa upande wake anatimiza majuku yake ipasavyo ili mtoto wake asiingie kwenye makundi hayo.

“Kuwa mwanaume ni heshima kubwa sana kama ukisimama kwenye misingi ya kiume..Nitauza vitumbua, madira hata kufagia barabara ilimradi mwanangu apate elimu,” alisema Shamsa.

Source: Bongo 5.
 
chawa ndiyo tabia gani?
 
nidsaidieni kujua Ford wa Kariakoo enzi zile anaishi au alishakufa
 
Duh hivi mumewe ana hio elimu anayoisemea? Anyway shamsa hivi unafahamu kuwa hao viben ten wengi ndo graduate wamekosa ajira miaka na miaka serikali haijatoa nafasi za kutosha so vijana wameamua kujiari kwenye umbea wapate hata matangazo watangaze kwa pesa. Je shamsa unafahamu hao unaowaita hawajasoma wengi ndo wanaongoza kwa pesa geukia chibu hana elimu ila kipaji na ujuzi vimemsaidia,geukia mpambe steve kila siku anapata dili mpya iwe rambi rambi,ukuwadi etc

All in all congrats kwa kujitambua kwenye malezi ya mwanao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…