Shamsa, Wellu Sengo ndani ya "BIFU" zito

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
STAA aliyeitendea haki Filamu ya Chausiku, Shamsa Ford na mwigizaji Wellu Sengo, wameingia kwenye bifu zito ambalo halijulikani chanzo chake.

Chanzo kimenyetisha habari kuwa, licha ya wawili hao kudumu kwenye urafiki kwa muda mrefu, ghafla wamebadilika na kwa sasa kila mmoja hamsemeshi mwenzake wanapokutana.

Jitihada za kumpata Shamsa ili kuzungumzia ishu hiyo hazikuzaa matunda lakini Wellu alipatikana:

"Unajua mimi niliona ghafla tu mtu hazungumzi na mimi, nikaona ni bora kuheshimu mawazo yake, mimi sijamkosea lolote sasa sijui ameninunia kwanini, " alisema Wellu.
 

Attachments

  • 1416092882548.jpg
    66.7 KB · Views: 2,892
hii sufulia (tasnia )ya bongo movie kiukweli inatia kinyaa japo wenyewe wanajiita na baadhi yetu kuwaita vioo vya jamii, mi nadhani wengi wao hawastahili kuwa hivyo ndio maana wenyewe kwa wenyewe hawaishi kukwaruzana.
Hata hili neno celebrity ah haya panapo kosekana bunduki rungu hufaa ki mtazamo wangu wengi hawastahili taji hilo, wanapenda tuwaone kama beyonce au kim kama sio jlo! dada zangu mnataka muishi kama hao wenzenu hawahongwi ni pesa yao nyie kwa pesa gani hii ya kucheza filamu bajeti yake 10m ?unauza sura unapewa laki tano? badilikeni. Ah nilitaka kusahau kama sio kunyang'anyana mabwana sidhani kama kuna jingine.
 
warumi uko single nini, usiku wa manane uko macho, au ulikuwa juu ya kiti kirefu?
 
Last edited by a moderator:

Hapo Shamsa lazima amchunie huyu mrembo maana akiwa nae karibu akawihii kumzidi kete maana demu ana kasura ka supu kama Seven.
 
Rafiki akikunyamaziaa nawe unamnyamaziaaa,maana rafiki sio oksijen kusema akikunyamazia hutapumuaa,,,Wellu mzurii balaaa
 
Au kahisi anataka kumuibia yule mumewe anayejishaua naye nini?
 
Mmh, mshaibiana mabwana, mfyuu ziwafikie popote mlipo, ile wellu kisu hatariii

Binamu huyo jb wanamgombania nasikia shamsa shoga yake kipenzi mke wa jb huku anamchukulia nasikia jb ni Noma kuna siku nilikua saluni wasaani wakanza kusemana wakasema jb mh wanamwaga mambo yao hadharani loh
 
warumi uko single nini, usiku wa manane uko macho, au ulikuwa juu ya kiti kirefu?

Jana mama yoyo alienda kupiga umbea kwa majiran mi kama kawa so tuligawana majukumu jana
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…