Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SHANTA GOLD MINE KUANZA KUMIMINA DHAHABU KUINEEMESHA IKUNGI, MBUNGE MTATURU AFUNGUKA
SHANTA gold mine sasa Kumimina Dhahabu kuineemesha Ikungi. Ni baada ya Kusimama kwa muda mrefu takribani miaka 19 tangu kusimama kwake sababu ikitajwa kuwa ni baadhi ya Wanasiasa kuweka vikwazo vilivyomfanya mwekezaji Kuutelekeza mgodi huo.
Akijibu Swali la Mwananchi wa Ikungi aliyeuliza kwa Mkuu wa Mkoa Wa Singida Mhe. Peter Serukamba, ni lini Shanta Gold mine itaanza kufanya kazi na kuwanufaisha wananchi, swali hilo ameliuliza mwananchi katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua uliofanyika wilayani hapo Februari 23, 2023 ambapo Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ameeleza kuwa sasa Mgodi huo utamimina dhahabu na kuineemesha Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kufuatia mapato yatakayopatikana katika Mgodi huo.
Vilevile pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba amesisitiza kuhusu mradi huo wa dhahabu unaotegemewa kuanza kumimina dhahabu kuanzia mwezi March 2023 kwa kuwataka wananchi kujiaandaa kimaendeleo naye alisema. “Ni lazima wananchi Tujiandaae kimaendeleo hii ni fursa kubwa, Halmshauri itapata fedha na mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa sana hapa wilayani kwetu, hali ya maisha ya watu itabadilika, lakini niwaombe msiwabeze wawekezaji mtaji wenu wa kwanza wanaikungi ni ardhi yenu”.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba Februari 23, 2023 amefanya kikao cha kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi wa Wilaya ya Ikungi kwa lengo la kuzitatua ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Ziara hii ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea Wilaya zote za Mkoa wa Singida kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Attachments
-
WhatsApp Image 2023-02-24 at 14.56.07(1).jpeg33.6 KB · Views: 12 -
WhatsApp Image 2023-02-24 at 14.56.06.jpeg29.8 KB · Views: 10 -
WhatsApp Image 2023-02-24 at 14.56.08(2).jpeg31.3 KB · Views: 10 -
WhatsApp Image 2023-02-24 at 14.56.09(2).jpeg44.2 KB · Views: 13 -
WhatsApp Image 2023-02-24 at 14.56.07(2).jpeg47.1 KB · Views: 9