Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) na kushika nafasi ya pili nyuma ya Mgombea wa CCM katika uchaguzi wa Jimbo la Kwahani Unguja (Zanzibar), Shara Amran Khamis, amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamo Mwenyekiti Zanzibar kupitia Chama cha ADC, amechukua fomu hiyo Juni 12, 2024 katika ofisi kuu za chama hicho Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Taifa wa chama hicho, Mwalimu Hamad Azizi, amemkabidhi fomu na kumuelekeza Shara Amran kufuata utaratibu wa kutafuta wadhamini kama kanuni za uchaguzi za chama hicho zinavyoelekeza.
Uchaguzi wa chama hicho unatarajia kufanyika tarehe 29 Juni 2024 katika Ukumbi wa Lamada uliopo Ilala, Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) alipochukua fomu katika ofisi kuu ya Chama cha ADC, Zanzibar.