๐—ฆ๐—ต๐—ฎ๐—ฟ๐—ฒ ๐—ถ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ป๐—ฒ๐˜๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐˜‚๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—•๐—น๐˜‚๐—ฒ๐˜๐—ผ๐—ผ๐˜๐—ต

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
Share intaneti kwa kutumia Bluetooth




Umeshawahi kutumia intaneti kwa mfumo wa Bluetooth kupitia simu yako ? Najua wengi tunaotumia simu kwenye mambo mengi tu ila wengi hatujui tunaweza share intaneti kwa kutumia Bluetooth.

Watu wengi tunatumia njia ya hotspot kuweza ku share intaneti kwenye vifaa vingine lakini sio lazima unaweza tumia Bluetooth kuweza kushare intaneti kwenye kifaa kingine kama vile simu , kompyuta pamoja na tablet.



Kwenye simu zetu Kuna kitu kinaitwa Bluetooth tethering, ni njia moja wapo ya kutumia mfumo wa wireless kuweza kusambaza upendo wa intaneti kwenye vifaa vingine kupitia Bluetooth.

Tusema una bando Kuna mtu anahitaji kushare na wewe kidogo sio lazima uwashe hotspot unaweza tumia tu Bluetooth kuweza kushare intaneti na wengine.

Wala uhitaji password kuweza kuunganisha kwenye ivyo vifaa unafanyaje ku share intaneti kwa kutumia Bluetooth kupitia simu yako ๐Ÿ‘‡
โ€ข ingia setting kwenye simu yako
โ€ข Kisha hotspot & tethering
โ€ข utagusa kwenye Bluetooth tethering
โ€ข hakikisha data Iko Kisha kwenye simu nyingine inahitajika kupata intaneti awashe tu Bluetooth ikishakua connected anaweza tumia intaneti bila password

Pia unaweza tumia njia hii kuunganisha na kompyuta yako kuweza kushare intaneti kwenye kompyuta kama upendi watu uwatajie password ya hotspot yako.

Umeshawahi kutumia hii njia au ndo unasikia Leo tuachie maoni yako ?
 
Sijasoma hata kusoma uzi wenyewe ila najua njia hizi nne za ku share internet kutoka kwenye android phone

1. Hotspot
2. Bluetooth tethering
3. Usb tethering
4. Ethernet tethering
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ