Share za Vodacom hazijapanda bei tangu ziuzwe kwenye IPO

Mzalendo07

Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
71
Reaction score
120
Hivi inaingia akilini mtu akikuambia VODACOM hawapati faida? Tangia wauze IPO kwa shilingi TSH 800/, Share zao hazijawai kupanda tena mpaka leo zimesimama kwa TSH 770/ na haziuziki. Hakuna mtu anazitaka hata kwa Tsh 600.

Hii maanaake ni nini? Ni kwamba hazina Value sokoni kwa kuwa azipandi thamani na VODACOM hawagawi mgawanyo wa FAIDA ata mara moja.

Cha kushangaza Serikali imekaa kimya, haijuwi jukumu lake ni kuwalinda wanainchi wasitapeliwa na kampuni kubwa kama hizi.
 
kibongo bongo kuwekeza kwa kununua shares za kampuni ni kuzika pesa yako tu.
 
Hivi inaingia akilini mtu akikuambia VODACOM hawapati faida? Tangia wauze IPO kwa shilingi TSH 800/, Share zao hazijawai kupanda tena mpaka leo zimesimama kwa TSH 770/ na haziuziki. Hakuna mtu anazitaka hata kwa Tsh 600.

Hii maanaake ni nini? Ni kwamba hazina Value sokoni kwa kuwa azipandi thamani na VODACOM hawagawi mgawanyo wa FAIDA ata mara moja.

Cha kushangaza Serikali imekaa kimya, haijuwi jukumu lake ni kuwalinda wanainchi wasitapeliwa na kampuni kubwa kama hizi.
Sasa serikali inaingiaje hapa? Wakat voda ni private firm na pesa zlizowekezwa na wawekezaji sio za SERIKALI?
 
Kuwa serious basi
Nipo serious mkuu, sijaelewa muunganiko wa serikali na anacholalamika mtoa mada, it's either haelewi ni vipi stock market inafanyakazi au ameamua tu kuilalamikia serikali (mana ndio hulka yetu wabongo wengi)
 
Sasa serikali inaingiaje hapa? Wakat voda ni private firm na pesa zlizowekezwa na wawekezaji sio za SERIKALI?

Mbona marekani SEC inaingilia haya maswala au na yenyewe sio serikali

Na kama umeangalia the wolf of wall street., ilikuwa inaelezea maisha ya stockbroker ordan bellfort aliyekuwa anatapeli watu kupitia penny stock,, ungewaona mpaka Fbi wanaingilia haya maswala wakipata wasiwasi juu yako
 
Ukisema Voda ni Private firm unakosea sababu ile ni PLC (Public Listed Company) kwa maana nyingine wamekusanya sehemu ya mtaji wao kutoka kwa UMMA.

Si kweli kwamba Voda hawapati faida, wanachokifanya wao wanatumia mapato wanayoyapata (faida) kukuza kampuni au kuongeza mtaji na hii ndo sababu wamekua wakisua sua kutoa gawio kila mwaka. japo kuna mwaka walitoa gawio kubwa kuliko kampuni yeyote iliyo listed DSE.

Suala la hisa zao kutopanda/kushuka bei iko hivi bei zinaongozwa na demand & supply kama hakuna wanunuzi ni dhahir bei itabaki ilivyo au kushuka ikiwa wapo watakao amua kuuza kwa bei ya chini.

Maono yangu pale voda watakavyobadilisha sera yao kuhusu faida wanayoipata na kuilekeza kwa wawekezaji kama CRDB tutaona bei ya hisa ikianza kupanda na kushuka kama yalivyo makampuni mengine.

Ukitaka hisa zinazouzika na bei inatembea vizur sokoni ni CRDB,NMB,TPCC ila muhimu kufanya uchambuzi wako uamue ni wapi uko tayari kuwekeza. Na unapowekeza usitarajie faida ya muda mfupi.
 
Hivi inaingia akilini mtu akikuambia VODACOM hawapati faida? Tangia wauze IPO kwa shilingi TSH 800/, Share zao hazijawai kupanda tena mpaka leo zimesimama kwa TSH 770/ na haziuziki. Hakuna mtu anazitaka hata kwa Tsh 600.

Hii maanaake ni nini? Ni kwamba hazina Value sokoni kwa kuwa azipandi thamani na VODACOM hawagawi mgawanyo wa FAIDA ata mara moja.

Cha kushangaza Serikali imekaa kimya, haijuwi jukumu lake ni kuwalinda wanainchi wasitapeliwa na kampuni kubwa kama hizi.
Tuwasiliane nizinunue, nitazinunua kwa 50% of the market price. Karibu.
 
Back
Top Bottom