Hii kwa waenga tu enzi hizo miaka hiyo TV zipo chache unakuta mtaa mzima ipo moja au hakuna kabisa na hapo mnaangalia ni mikanda tu na wenye nyumba wakali maana watoto kwa kuchafua nyumba na miguu michafu basi mnasema kesho usiwafungulie hahahaaha
Na jirani yangu huku kitaa yeye marufuku yake watoto wasiingie ndani bali wachungulie dirishani Dah roho huwa inaniuma sana lakini chakushangaza watoto wanafurahia hiyo hali na wala hawanung'uniki nikagundua utoto raha sana.