Sharti Mbunge awe amepitia JKT au jeshini na amewahi kutumikia taifa

Sharti Mbunge awe amepitia JKT au jeshini na amewahi kutumikia taifa

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
Kama ilivyo kwa ajira nyingine ambazo kigezo mojawapo ni ukakamavu na uzalendo (JKT).

Tunahitaji MBUNGE sifa ya kugombea iwe JKT na awe na historia ya KUTUMIKIA TAIFA kwa uzalendo kwa muda usiooungua miaka mitano.
 
Naunga mkono hoja kwa 100%

Ili taifa liweze kupunguza idadi ya mamluki!

Ingawa sio suluhisho la kuwapandikiza uzalendo!

Sababu tatizo kubwa ni wengi kuendekeza tamaa binafsi na kujitajirisha kwa njia za mkato!

Na tamaa haichagui baina ya mzalendo na mamluki sababu Tamaa ni mojawapo ya maumbile ya binadamu toka anazaliwa sambamba na njaa!

Sasa hawa wabunge wetu wengi wanaiendekeza tamaa kutokana na njaa za kujishibisha ukwasi.
Ahsante.
 
..kuna watu wako juu ya sheria.

..hao ndio wanaoharibu mfumo mzima wa utawala nchini.

..tutunge sheria kila, na kila mmoja aguswe na sheria hizo.

..pia tuwe wakali ktk kuzilinda sheria hizo ili zisivunjwe.

..tuwe na BUNGE lenye meno. Bunge hilo ni lile ambalo halina ukiritimba wa chama kimoja.

..Mwisho tuwe na mahakama iliyo huru.
 
Ujinga tuu. Kikwete, kinana na wengine wengi wamepita jeshini tena wamepata na vyeo lakini wamekuwa wezi wakubwa tuu kwenye hii nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom