Mawakili wanajua kula pesa watejaMahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imeondoa shauri la awali lililofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, maarufu kama Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima.
Maombi ya kuondoa shauri hilo yaliwasilishwa na waleta maombi kupitia kwa Wakili Peter Kibatala akiwakilishwa na Wakili Alphonce Nachipyangu, baada ya Serikali kuwasilisha barua rasmi na sahihi inayomtaja mteja wao kwa jina sahihi ambalo linatambulika kisheria.
Akizungumza mara baada ya uamuzi huo wa Mahakama Julai 14, 2025, Wakili Nachipyangu amesema:
“Hoja yetu ilikuwa ni kuondoa yale maombi ya awali ambayo tuliyaleta tangu mwanzo ili tuweze kuwasilisha upya maombi sahihi. Tulifika Mahakamani kwa mara ya kwanza kutokana na barua tuliyoiona mitandaoni, ambayo tuliona ina mapungufuhaikumtaja mteja wetu kwa usahihi na pia haikusainiwa. Hata hivyo, wakati tukiwa Mahakamani, Serikali iliwasilisha barua nyingine rasmi ambayo sasa inamtaja mteja wetu vile tunavyomtambua kisheria.” amesema Wakili Alphonce, Shauri hilo lilifunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa kanisa hilo kufuatia hatua ya Serikali ya kulifungia kanisa hilo.
Itakumbukwa kuwa Juni 2, 2025, waumini wa kanisa hilo walizuiwa kufanya ibada katika makanisa yao, baada ya vyombo vya dola kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya taasisi hiyo ya kidini.
Wakili Alphonce amesema kuwa baada ya kuondolewa kwa shauri hilo, wanatarajia kuwasilisha maombi mapya Mahakamani kwa kufuata taratibu zote stahiki. Shauri hilo lilikuwa linasikilizwa Mahakamani hapo mbele ya Jaji Juliana Masabo
Hii nchi tuna uongo afu tuna wizi.....
Kwa sababu ndiyo hiyo inayotumiwa na serikali hiyo hiyo kupitia jeshi la polisi kusababisha athari za waumini wa kanisa la GCTC.Mawakili wanajua kula pesa wateja
Unatumiaje barua uliyooona mtandaoni kufungua mashitaka?
Hawajawahi kupewa barua yoyote kwa njia yoyote zaidi ya hiyo ya mtandaoni.Badala ya kuwaomva wateja wakupe barua halisi waliyopewa na msajili kwa despatch?
Hakuna wizi wowote hapo. Ni utaratibu wa kawaida wa kisheria uliofuatwa na kanisa kuweka mambo sawa...Wizi mtupu.Hapo wameshawachukulia pesa kibao hao waumini wa Gwajima wasiojua sheria
Kwani hao wanaotekeleza amri hiyo iliyotolewa kupitia barua hiyo wao wanatumia barua gani?Hata kwa akili za kawaida tu wakili unaulizwa hiyo barua unafungulia kesi uliitoa wapi ? Unajibu mtandaoni
Serikali imefanya kosa na itashindwa mchana kweupe kwenye kesi..Wakili Kibatala Mungu anakuona ujue
Acha uongo wewe afisa wa serikali na mkuu wa wilaya walienda kukabidhi barua tena kwa despatchHawajawahi kupewa barua yoyote kwa njia yoyote zaidi ya hiyo ya mtandaoni.
Wazo lilikuja
Mawakili wanajua kula pesa wateja
Unatumiaje barua uliyooona mtandaoni kufungua mashitaka? Badala ya kuwaomva wateja wakupe barua halisi waliyopewa na msajili kwa despatch?
Wizi mtupu.Hapo wameshawachukulia pesa kibao hao waumini wa Gwajima wasiojua sheria
Hata kwa akili za kawaida tu wakili unaulizwa hiyo barua unafungulia kesi uliitoa wapi ? Unajibu mtandaoni
Wakili Kibatala Mungu anakuona ujue
Dkt Samia akitoka madarakani, mtamkumbuka sana
Ghafla sanaWazo lilikuja
Sio ishu ya uongo hapa..Acha uongo wewe afisa wa serikali na mkuu wa wilaya walienda kukabidhi barua tena kwa despatch
Walikataa? Halafu ukachukua hatua gani? Walipeleka hata kwa serikali ya mtaa lilipo hilo kanisa? Eeh, ikawaje..?Gwajima na uongozi wake wakakataa kupokea hiyo barua original kwa mkono officially .
Wakili gani ambane nani?utoto wakili kama sio mpenda pesa alitakiwa kuwabana kwa nini hamkupokea barua original? Kawalia pesa zao bure kwa kitu kidogo tu wangepokea ile barua original kesi ingeendelea vizuri sasa ona kitendo chao cha kukataa kupokea barua originali .Mawakili wanaanza kesi upya baada ya kulamba pesa kwa kesi hewa ya mwanzo
Huyu mpumbavu huyu, mshirika wa uhuni nani amsikilize?Msikilize mkuu wa wilaya akiongea kuhusu barua original
View: https://youtu.be/-cRt45zOdPQ?si=fgYOt6qoSnc0a10v