Daddo
JF-Expert Member
- Jan 17, 2013
- 1,435
- 1,025
Mimi sijambo kabisa na natumai hata wewe unayesoma haujambo.
Najua unajishangaa kusoma bandiko kama hili maana halina kitu chochote cha msingi isipokuwa kukupotezea muda tu.
Kwakuwa sitaki uzidi kukasirika na kujutia kufungua uzi huu basi ngoja tu nikwambie ukweli kwamba hii mada haikuhusu kabisa bali namuhusu mwana Jf mwenzako mwenye tabia hii hapa chini ninayotaka kuielzea. Nitabia gani basi niliyoilenga usiku huu? Nisikuchoshe sana fatana na mimi;
Ebwana kumekuwa na mtindo fulani kwenye jamii hii ya wanaojiita Great thinkers kuchukuliana wa-ke/me huku wakijua kwamba kwa namna moja au nyingine hilo swali linaweza kuleta matatizo au madhara fulani mbeleni lakini wakaamua kujivalisha miwani nyeusi na kuact kama hawajui hivyo kukamilisha azma yao kwa moyo mkunjufu kabisa.
Mimi kinachonishangaza sasa wakati mamlaka ya kichwa cha mtenda jambo inapoamua kufanya hivyo huwa haishirikishi Jf. Hufanya hivyo kimyakimya na kwa usiri mkubwa lakini sasa mambo yanapoharibika huko badala ya kukabiloana nayo wanakimbilia kutafuta ushauri Jf. Utasikia, "oooh jamani yamenikuta nimetembea na bosi wangu amenipa/nimempa mimba na mimi nina m-me/ke naombeni ushauri", khaa! Unatuomba ushauri gani kwani tulikushauri uende kufanya hivyo?, wakati unafanya ulikuwa hujui kama inaweza kutokea?, kuna mtu alikufunga kamba kwenda kulala na mpenzi wa mwenzako?, ulikuwa hujajiandaa kukabiliana na kitakachotokea?
Ngoja basi nikunje jamvi nitoke uwanjani ila usijisifu wewe unayechukua watoto wa shule kwamba sijakugusia la hasha hapa nikezungumzia kitu kimoja lakini kwa mwenye akili atajua kwamba nimegusia sehemu zote ambazo mtu anafanya kitu kibaya kwa makusudi linapotokea la kutokea anahaha kutafuta wa kumlaumu, wapenda ma hause girl, wapenda watoto wa wenzenu kwa kigezo kwamba mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzako wote mko kwenye kundi moja.
Ushauri tu ni kwamba aga kwanza Jf uweke nia yako na uombe ushauri wa kile unachotaka kukifanya then Jf wakikushauri kukifanya kafanye ili yakikukuta uje kuomba ushauri wa kukabiliana na hiyo outcome(s). Vinginevyo naona wana J tunawajibishwa kwa makosa yasiyokuwa yetu.