mimi sishangai, wako wengi wa aina hiyo, tena wenye degree zao, anakueleza kitu mwanzo hadi mwisho lakini huelewi anataka kukuambia nini, muda mwingine ili usimuulize ulize sana inabidi uunge unge mwenyewe mpaka ukamilishe hadithi yenyewe kwa uelewa wako. huyu hana tofauti na yule anakueleza mambo 10 lakini yote yameishia katikati. maana akianza hili, hajamaliza, karukia lingine, halijaisha nalo, ghafla anaanza story nyingine, ili mradi aongee na kukufanya usikilize mambo nusu nusu. ndivyo alivyo huyo. sidhani kama kuna jinsi ya kumsadia abadilike, hata ukimlaumu hatakuelewa maana anajiona yuko sawa.