Sheffield United yaendelea kusalia nafasi za mwishoni

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105

Sheffield United ikiwa nyumbani imelazimishwa kichapo cha goli 1 kwa 0 na vijana wa Pep Guardiola, Manchester City katika Dimba la Bramall Lane

Huu ni mwendelezo wa matokeo mabaya kwa Sheffield baada ya kupoteza michezo sita na kusuluhu mchezo mmoja kati ya michezo 7 ambayo imekwisha kucheza tangu msimu kuanza na kushika nafasi ya 19 juu ya Fulham ambaye anashika nafasi ya 20

Klabu hiyo ambayo ilitambuliwa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) kuwa klabu kongwe zaidi, ilikuwa na mafanikio makubwa katika msimu wa 2018-2019 na hatimaye kupanda daraja na kushiriki Ligi kuu kwa mara nyingine baada ya kushushwa daraja kwenye Msimu wa 2006-2007

Kwa upande wa Manchester City, imejinyakulia alama 3 katika mchezo huo ambazo hazijaiwezesha klabu hiyo kutoka nafasi moja kwenda nyingine baada ya kuendelea kusalia katika nafasi ya 7 ya msimamo wa ligi hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…