- Thread starter
-
- #21
MUHTASARI WA SOMO LA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA 1 - IV 2023
Utangulizi
Somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu ni moja ya masomo chaguzi katika Elimu ya Sekondari Kidato cha I – IV kwa wanafunzi walioko katika Mkondo wa Elimu ya Jumla.
Somo hili linalenga kumjengea mwanafunzi maarifa, stadi na mwelekeo ikiwemo kutumia Aya na Hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W) zilizoteuliwa kumwezesha kukabiliana na mazingira yanayomzunguka
katika maisha ya kila siku.
Aidha, ujifunzaji wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu utakuza uwezo wa mwanafunzi kufahamu aina za Tawhid, ibada za Faradhi na Sunnah, matendo mema na kufanya kazi za kiuchumi na kutumia mali kwa usahihi, kuiga matendo ya Mtume Muhammad (S.A.W) na Maswahaba zake waongofu katika maisha ya kila siku.
Aidha, mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kumuabudu Mola wake kwa usahihi pamoja na kuitumikia jamii katika nyanja mbalimbali.
Mwanafunzi pia atakuwa mahiri wa kujitolea, kushirikiana, kuwa mzalendo, kudumisha umoja na kuipenda nchi yake kwa kuzingatia misingi ya Uislamu na kulinda amani ya eneo lake na nchi kwa ujumla.
Aidha, Muhtasari umeandaliwa ili kuongoza ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu Elimu ya Sekondari Kidato cha I - IV katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Muhtasari huu unatafsiri umahiri uliobainishwa kwenye Mtaala wa Elimu ya Sekondari Kidato cha I - IV wa Mwaka 2023. Muhtasari unatoa maelekezo ya kuwawezesha walimu kuandaa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji kwa ufanisi.
Vilevile, muhtasari unatoa nafasi kwa Mwalimu kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu zitakazokuza stadi za karne ya 21 zikiwemo ubunifu, mawasiliano, ushirikiano.
2.0 Malengo Makuu ya Elimu Tanzania
Malengo makuu ya elimu nchini Tanzania ni kumwezesha kila Mtanzania:
(a) Kukuza na kuboresha haiba yake ili aweze kujithamini na kujiamini;
(b) Kuheshimu utamaduni, mila na desturi za Kitanzania, tofauti za kitamaduni, utu, haki za binadamu, mitazamo na matendo jumuishi;
(c) mtazamo chanya katika maendeleo yake binafsi na maendeleo endelevu ya taifa na dunia kwa ujumla;
(d) Kuelewa na kulinda tunu za taifa ikiwa ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uaminifu, uwajibikaji na
lugha ya Taifa;
(e) Kujenga stadi za maisha na stadi za kazi ili kuongeza ufanisi katika maisha ya kila siku;
(f) Kukuza tabia ya kupenda na kuheshimu kazi ili kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji na utoaji wa huduma;
(g) Kutambua na kuzingatia masuala mtambuka ambayo ni pamoja na afya na ustawi wa watu (jamii), usawa wa kijinsia,
usimamizi na utunzaji endelevu wa mazingira; na
(h) Kukuza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa, amani na haki kwa kuzingatia katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa.
3.0 Malengo ya Elimu ya Sekondari Kidato cha I – IV - Elimu ya Jumla Malengo ya Elimu ya Sekondari Kidato cha I – IV Elimu ya Jumla ni:
(a) Kuimarisha, kupanua na kuendeleza uelewa wa kina wa maarifa, stadi na mwelekeo alioupata katika hatua ya Elimu
ya Msingi;
(b) Kulinda mila na desturi, umoja wa kitaifa, tunu za taifa, demokrasia, kuthamini haki za binadamu na za kiraia, wajibu
na majukumu yanayoendana na haki hizo;
(c) Kukuza tabia ya kujiamini na uwezo wa kujifunza kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo sayansi na teknolojia,
maarifa ya kinadharia, na kiufundi;
(d) Kuimarisha mawasiliano kwa kutumia stadi za lugha ikiwemo Lugha ya Alama ya Tanzania (LAT), lugha mguso, lugha ya Kiswahili, Kiingereza na angalau lugha moja nyingine ya kigeni;
(e) Kuimarisha uwajibikaji katika masuala mtambuka ya kijamii yakiwemo afya, usalama, usawa wa kijinsia na utunzaji
endelevu wa mazingira;
Soma zaidi Somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu
Source : tovuti ya tie.go.tz -Taasisi ya Elimu Tanzania