Shehena ya bidhaa toka Kenya zakamatwa na kuteketezwa kwa moto.

Shehena ya bidhaa toka Kenya zakamatwa na kuteketezwa kwa moto.

Ashura9

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Posts
740
Reaction score
485
Shehena ya bidhaa mbalimbali zenye viambata vyenye sumu ikiwemo dawa, vipodozi, vinywaji na vyakula ambavyo baadhi yake ni kutoka nchi jirani ya Kenya, vimekamatwa kisha kuteketezwa kwa moto baada ya kubainika kuwa vimeingizwa nchini na kuuzwa wakati muda wake umekwisha na hivyo kuhatarisha afya za watumiaji.

moto10%282%29.jpg

Bidhaa hizo zenye uzito wa tani 2.5 zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 14.2, zimekamatwa katika maeneo tofauti ikiwemo Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania huku nyama na baadhi ya vinywaji ambavyo vilikuwa vikiuzwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na muda wake wa matumizi umekwisha vimekamatwa jijini Tanga.

Akielezea jinsi wageni kwa kushirikiana na watanzania wanavyopitisha bidhaa hizo na kuingia nchini bila kufanyiwa ukaguzi, mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa mamlaka ya chakula na dawa tawi la Horohoro Bwana Thomas Nkondola amesema baadhi yao wamekuwa wakipitisha shehena ya bidhaa zilizoharibika kupitia katika mabasi yanayofanya safari zake kutoka Mombasa kuja nchini hatua ambayo imekuwa ikikwamisha zoezi hilo.

Kufuatia hatua hiyo afisa afya anayeshughulikia usalama wa chakula na lishe wa halmashauri ya jiji la Tanga Alice Maungu amewatahadharisha
wananchi kuwa makini mara wanaponunua vinywaji na bidhaa aina ya vipodozi kuhakikisha wanakagua tarehe za matumizi kabla ya kununua ili kuepuka madhara kwa mtumiaji.
 
Back
Top Bottom