Shehu Shaghari

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
ALHAJ SHEHU USMAN ALIYU SHAGARI; RAIS WA KWANZA KUCHAGULIWA KIDEMOKRASIA NCHINI NIGERIA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu
Friday-4/1/2019.

Mapema siku ya tarehe 28/12/2018 mjukuu mkubwa wa rais wa Saba wa Nigeria Alhaj Shehu Usman Aliyu Shagari anaeitwa Bello Shagari aliutangazia umma kupitia akaunti yake ya Twitter juu ya kifo cha babu yake ambacho kilitokea kwenye hospital kuu ya taifa ya jijini Abuja aliko kuwa akipatiwa matibabu yanayotokana na uzee na umri mkubwa. Kupitia akaunti hiyo Bello Shagari, aliandika... “I regret announcing the death of my grandfather, H.E Alhaji Shehu Shagari, who died right now after brief illness at the National hospital, Abuja,”

Kufatia kifo hicho nilihaidi kuwaletea makala juu ya historia nzima ya Shehu Shagari rais wa kwanza wa kiraia kuchaguliwa baada ya mzuka wa mapinduzi ulioikumba Nigeria mara baada ya uhuru wake mapema mwaka 1960.

Baada ya Nigeria kupata uhuru wake tu mwaka 1960, Rais wa kwanza wa nchi hiyo Benjamin Nnamdi Azikiwe alipinduliwa na Meja Jenerali Johnson Aguiyi-Ironsi mwaka 1966, katika kipindi cha mapinduzi hayo Alhaj Abubakar Tafawa Balewa waziri mkuu wa kwanza wa serikali ya shirikisho la Nigeria aliuwawa na wafuasi wa Meja Jeneral Johnson Aguiyi-Ironsi, Meja Jeneral Johnson nae akudumu madarakani kwani nae alikuja kupinduliwa na Jenerali Yakubu Gowon mwaka huohuo. Zimwi la mapinduzi liliendelea kwani hata Jenerali Gowon nae alipinduliwa mwaka 1975 na Jenerali Murtala Mohammed.

Pinduapindua hiyo iliendelea hadi mwaka 1976 baada ya vita mbaya ya wenyewe kwa wenyewe iliyoitwa "Machafuko ya kujitenga kwa Biafra"Kumalizika, baada ya Meja Jenerali Olusegun Obasanjo kumpindua Jenerali Murtala Mohammed. Lakini baada ya miaka mitatu ya uongozi wake, Jenerali Obasanjo aliamua kujiuzulu ili kupisha uchaguzi huru utakaoiwezesha Nigeria kupata Rais wake wa kwanza wa kidemokrasia anayetokana na uchaguzi wa kiraia.

Na hapa ndipo alipochaguliwa Alhaj Shehu Shagari aliyefariki juzi December 28 mwaka 2018. Shagari anayetoka kaskazini mwa nchi hiyo alikabiliwa na upinzani kutokana na mgogoro wa mafuta na hivyo mwaka 1983 akapinduliwa na Jenerali Muhammadu Buhari (ambaye sasa ni Rais wa taifa hilo ambae awamu hii ameingia kwa njia ya demokrasia).

Shehu Shagari ambae tutamuangazia leo anakumbukwa kuwa moja ya maraisi walio fungua uchumi wa sasa wa Nigeria, pia alikuwa kiongozi wa mwanzoni kabisa nchini Nigeria aliyehudumu serikali zote za awali toka uhuru aliye kuwa amebakia hai. Makala hii ndio makala yangu ya kwanza kuandika kwa mwaka huu wa 2019. Kufatia umuhimu wa Shagari nchini Nigeria nimeona ni vyema tujifunze na kumfahamu rais huyu mpole,masikini na ambae akujilimbikizia mali kuliko marais wote Nigeria.

Shehu Usman Aliyu Shagari alizaliwa mwezi Februari 25, 1925 na kufariki dunia mwezi Desemba 28, 2018 siku mbili baada ya sikukuu ya Xmas na siku tatu kabla ya kuuona mwaka mpya huu wa 2019 Shagari amefariki akiwa na umri wa miaka 93, Shagari alikuwa mwanasiasa wa Nigeria ambaye aliwahi kuwa Rais wa kwanza kuchaguliwa kwenye uchaguzi wa kidemokrasia nchini Nigeria na wa pekee wa Jamhuri ya pili ya Nigeria toka mwaka 1979 mpaka mwaka 1983, baada ya kuchaguliwa alihudumu kama rais na baadae kupinduliwa kwa nguvu na Mkuu wa majeshi wakati huo Muhammadu Bahari ambae ndio rais wa sasa.

Shagari pia alitumikia serikali ya Nigeria mara saba katika nafasi ya waziri au ya baraza la mawaziri kama waziri wa shirikisho kutoka 1958 wakati wa serikali ya kikoloni mpaka mwaka 1975 kipindi cha serikali ya kwanza ya uhuru iliyo ongozwa na Benjamin Nnandi Azikiwe na walio mfuata.

Shagari aliteuliwa kuwa Turaki wa eneo la Fula Sokoto mwaka 1962 na Sultan wa Sokoto aliyeitwa Siddiq Abubakar III. Neno "Turaki" ina maana ya afisa maalumu katika mahakama za kidini huko Nigeria, katika kusimamia kesi na ustawi wa mahakama hizo za sultani katika utawala wa kichifu huko Sokoto. Aidha, shagari amewahi kuwa Chief aliyetekeleza majukumu ya kiutawala kwenye jamii ya Ochiebuzo ya Ogbaland, na kuongoza jamii ya Waislamu wa Aboucha na Baba Korede wa Ado Ekiti huko kaskazini mwa Nigeria.

Huyu Alhaj Shehu Usman Shagari alizaliwa katika kijiji cha kaskazini cha Shagari kilichoanzishwa na babu yake mkubwa aliyeitwa Ahmadu Rufa'i, ambaye pia alikuwa Mkuu wa kijiji hicho, Shagari alipozaliwa babu yake akaamua kumwita jina la kijiji hicho "Shagari".Alilelewa na kukulia katika familia ya mitaala (polygamous family), na alikuwa ni mtoto wa sita kuzaliwa katika familia ya mzee Aliyu Shagari.

Shagari alianza elimu yake katika shule ya masomo ya Qur'an kisha akaenda kuishi nje kidogo na kwao kwa ndugu zake kwa ajili ya kupata elimu ya msingi, ambapo kutoka 1931 mpaka 1935 alihudhuria shule ya msingi ya Yabo. Na mwaka 1936 mpaka 1940, alikwenda eneo la Sokoto kwa ajili ya kusoma shule ya kati, na kisha mwaka 1941 hadi 1944 alihudhuria Chuo Kikuu cha Kaduna. Kati ya mwaka wa 1944 na 1952, Shehu Shagari, akiwa katika Chuo cha Mafunzo ya Ualimu, huko Zaria, Kaduna, Nigeria. Kuanzia mwaka 1953 hadi mwaka 1958, alipata kazi kama mwalimu katika Mkoa wa Sokoto. Pia alikuwa mwanachama wa Bodi ya Shirikisho la ufadhiri (Scholarship) tangu 1954-1958.

Shagari aliingia katika siasa mwaka wa 1951, alipokuwa katibu wa balaza la Watu wa kaskazini huko Sokoto, nafasi aliyo ishikilia mpaka 1956.

Mwaka 1954, alichaguliwa katika ofisi yake ya kwanza ya umma kama mwanachama wa Baraza la Wawakilishi wa Shirikisho la Sokoto magharibi. Mwaka wa 1958, Shagari alichaguliwa tena kuwa katibu wa bunge (alihudumu nafasi hiyo hadi mwaka 1959) chini ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Nigeria, Sir Abubakar Tafawa Balewa na mwaka huo pia alihudumu kama Waziri wa Fedha na Viwanda kwenye serikali ya muda wakati maadalizi ya uhuru yakielekea ukingoni.

Kuanzia 1959 hadi 1960, Shagari alihamishiwa katika nafasi ya kiuchumi, kama Waziri wa Shirikisho wa Maendeleo ya Uchumi. Kutoka 1960 hadi 1962, alihamia huduma ya Pensheni kama Waziri wa atakaye shughurikia maswala ya Pensheni. Kuanzia 1962-1965, Shagari ilihamishiwa wizara ya ndani na kufanya kazi kama waziri wa Shirikisho kwa masuala ya ndani. Kuanzia mwaka wa 1965 mpaka mapinduzi ya kwanza ya kijeshi Januari 1966, Shagari alikuwa ni waziri wa Shirikisho anaye husika na maswala ya kazi.

Mwaka 1967 alichaguliwa kuwa katibu wa mfuko wa maendeleo ya elimu ya jimbo la Sokoto. Kuanzia mwaka wa 1968-1969, alipewa nafasi ya uangalizi na usimamizi katika Jimbo la Kaskazini Magharibi kama kamishna wa jimbo kufatia kuongezwa kwa majimbo mengine nchini humo.

Kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Nigeria, tangu 1970 hadi 1971, Shagari ilichaguliwa na kiongozi wa kijeshi na serikali wakati huo Jenerali Yakubu Gowon kuwa kamishna wa shirikisho wa maendeleo ya uchumi, ukarabati na ujenzi. Katika serikali ya kijeshi iliyochukua nchi. Kuanzia 1971 hadi 1975 aliteuliwa kuwa Kamishna wa Shirikisho wa fedha (nafasi ambayo ndio inayoitwa waziri kwa sasa). Wakati wa utumishi wake kama Kamishna wa Fedha wa Nigeria, Shagari pia alikuwa ni mjumbe wa gavana wa Benki ya Dunia na mwanachama wa Kamati ya Kimataifa ya Fedha (IMF).

Mnamo 1978 kufatia serikali ya kijeshi iliyokuwa ikiongozwa na Olusegan Obasanjo kuitisha uchaguzi wa kiraia, Shehu Shagari akajitosa kwenye siasa kwa lengo la kuwania nafasi ya urais na kuamua kuunda chama cha siasa na alikuwa mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Taifa cha Nigeria (NNP). Mwaka ulio fuata yani mwaka 1979 Shagari alichaguliwa na chama chake kama mgombea wa urais wa uchaguzi mkuu ulio itishwa mwaka huo, hata hivyo Shagari katika uchaguzi huo alishinda na kuwa rais na mkuu wa nchi ya Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria.

Shagari alichaguliwa tena kwa kipindi cha pili cha miaka minne mwaka 1983 na alishinda uchaguzi mkuu, hata hivyo, Desemba 31, 1983, Shagari alipinduliwa na Maj. Gen. Muhammadu Buhari.

Katika utawala wake aliongeza uzalishaji na uvumbuzi wa mafuta, Shagari alishughulikia tatizo la Nyumba kwa raia wake kwa kujenga Nyumba, alitanua sekta ya Viwanda, Usafiri na Kilimo kote nchini malengo makuu ya utawala wake ulikuwa ni Katika sekta ya usafiri, alizindua baadhi ya mitandao ya barabara kote nchini. Pia alianzisha mpango wa matumizi ya mitambo ya kisasa katika kilimo. Mpango huu uliwanifaisha na kuwapendelea zaidi wakulima wakubwa. Shagari pia alianzisha mpango wa makazi ya gharama nafuu kote nchini.

Mwaka wa 1980, pamoja na mapato ya mafuta kuongezeka, Shagari alimaliza ujenzi wa kituo Kikubwa cha kusafishia mafuta (raffinery) cha Kaduna, ambacho kilianza kufanya kazi mwaka huo huo. Shagari pia ilihitimisha ujenzi wa viwanda vya chuma na vituo vitatu vya kusambaza nishati ya umeme huko Ajaokuta. Alikamilisha kiwanda kikubwa cha Steel kilichoitwa Delta Steel complex industry mwaka 1982. Mwaka uliofuata yani mwaka 1983, Shagari aliunda Kampuni ya Aluminium Smelter ya Nigeria huko Ikot Abasi.

Serikali ya Shagari ilianza mpango wa kuhifadhi mazingira uliojulikana kama "Mapinduzi ya Green", ambapo serikali yake ilitoa mbegu na mbolea (fertilliser) kwa wakulima kuongeza upandaji wa miti na uzalishaji wa kilimo katika taifa.

Kuanguka kwa bei ya mafuta ambayo ilianza mapema mwaka 1981 iliathiri sana mzunguko wa fedha za serikali ya shirikisho la Nigeria. Kufatia hatua hiyo Shagari alianzisha Programu ya Uimarishaji wa Uchumi ili kusaidia kulinda na kufufua nchi dhidi ya kuporomoka kwa soko la mafuta sekta inayochangia kiwango Kikubwa cha pato la taifa nchini Nigeria. Mpango huo ulifanikiwa kutatua mdororo wa uchumi na kupelekea uchumi kukuwa kwa kiwango cha juu cha miaka ya 1970 na kuifanya Nigeria kuongoza katika ukuaji wa uchumi kwa kiwango kizuri katika ukanda mzima wa Afrika ya magharibi.

Hatua muhimu alizo chukua Shagari kipindi hicho katika mpango huo ilikuwa ni ni kupunguza leseni za kuagiza bidhaa njee kuruhusu ukuaji wa viwanda vya ndani, kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza ushuru wa utoaji mafuta ghafi nje ili kuvipa nafasi viwanda vya kuchakata mafuta ghafi vya Kaduna na Port Haikort ili kuongeza thamani ya uzalishaji wa ndani. Hata hivyo, bei ya mafuta Iliendelea kupolomoka zaidi duniani hatimae matokeo ya mipango hiyo ya ufufuaji wa uchumi ilianza kuleta matokeo chanya kwa kiasi kidogo Sana baadae.

Kufatia hatua hiyo ya ufufuaji uchumi kushindwa kufufua uchumi kwa kasi kufatia kuendelea kuporomoka kwa bei ya mafuta, Utawala wa Shagari ukaanza kuwa na mashaka kubwa katika kundesha nchi kufatia ukame mkubwa wa pesa kwa serikali yake hatimae rushwa ikaanza kuchomoza kwa kasi, ikiwa ni pamoja na madai ya udanganyifu wa uchaguzi katika uchaguzi wa 1983. Hii, pamoja na kushuka kwa bei za mafuta duniani, na kuzorota kwa mzunguko wa fedha za kitaifa, shida ya upatikanaji wa huduma kwa wananchi, ikasababisha serikali yake kuwa na mgogoro na wananchi. Kufuatia hali hiyo serikali ya Shagari ilipinduliwa na Mkuu wa majeshi wa wakati huo Muhammadu Buhari katika mapinduzi ya kijeshi yaliyo tekelezwa tarehe 31 Desemba 1983.

Shehu Shagari alioa wake watatu ambao ni Amina, Aishatu na Shagari Hadiza. Na alikuwa na na watoto wengi. Mapema mnamo Agosti 24, 2001 mkewe, Aisha Shagari, alifariki akiwa hospitali ya London nchini Uingereza baada ya kuugua ugonjwa kwa muda mfupi.

Alhaj Shehu Shagari aliaga dunia Desemba 28, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Nigeria jijini Abuja alipo kuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa kijiji kwao Sokoto saa 2:26 mchana kwenye ghofu la nyumba yake iliyopo huko kijijini kwao, tarehe 29/12/2018, umauti ulimkuta Shehu Shagari akiwa na umri wa miaka 93.


Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…