Vuguvugu la uchaguzi limeleta mambo mengi sana mwaka huu. Kati ya hayo mojawapo ikiwa ni viongozi wa dini kutupiana maneno hadharani. Uhasama kati ya viongozi hawa wawili ulianza pale sheikh Alhad Mussa alivyomuombea dua ya "kipekee" mgombea wa urais kupitia CCM, John Magufuli. Hata hivyo nimefurahishwa na kitendo cha hawa viongozi wawili wa dini kwa kumaliza tofauti zao hadharani.
View attachment 1611749
Kwa kumchana ambako alhadi alimchana abuu iddi basi abuu iddi katumia busara sana kutaka yaishe maana alhadi yeye lengo lake ilikuwa ampasue kabisa kabisa amuweke hadharani.
Abuu iddi katika kauli zake juu ya dua ya alhadi kuna maneno aliongea ambayo yalitafsiriwa na watu kwamba pengine anaona alhadi hatoshi,mpaka ikafikia hatua akahoji kaupatia wapi huu ushekhe wa mkoa,alhadi alichukia sana hili jambo..
Pia kumnukuu kwa makosa alhadi kuwa ati kasema Mingu alipoumba kuna wakati alipumzika,abuu iddi akasema kuwa alhadi anafanya istihzaai kwa amungu huyu mtu,wakati huo alhadi alishasema kuwa "KUNA REDIO MBAO ZINASEMA HIVYO..
Kwa maana neno redio mbao alhadi mwenyewe alikusudia kuwa yale msneno sio sahihi,abuu iddi akanukuu kwa makosa kuwa ati alhadi kasema hivyo.
Sasa kamzulia jambo hili alhadi pia kamaind sana kwamba lengo lake nini huyu jamaa ?
Alhadi akaona amtolee uvivu akamchana na kutoa ya moyoni ambayo pia watu wametafsiri kuwa pengine alhadi naye alikuwa anamuona abuu iddi tokea muda anakengeuka kutokana na kuwasema sema mashekhe
Kitokana na dhana hizi za watu nadhani imekuwa busara kwao sana kuyamaliza na kusonga mbele.kwa sababu nina imani kama imgekuwa chana nikuchane mwisho wa siku wangetoleana aibu tu kwa sababu naamini wanajuana.
Lakini kwa upande wangu naona abuu iddi kama anajihusisha mna baraza la ulamaa basi anatakiwa asiwe mwepesi kuwasema mashekhe wenzake kwa sababu ile sio sifa nzuri ya kuwa kiomgozi.
Lakini funzo lingine ni kuwa ukigomvana na mtu hata kama unayajua mabaya yake na yale asiyoyapenda kujihusu yeye(ya aibu)basi usiyaseme katika ule ugomvi maadamu tu ugomvi wenu hauhusiani na aibu hizo.
Kudhibiti maneno wakati wa magomvi na hasira ni hazina yenye kukupa ushindi hata pale utakapoanguka.