Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 26, 2026, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania (JMAT) Taifa, Sheikh Alhad Mussa Salum, amesema;
"Kwenye uchochezi wowote wa namna yoyote ile, uwe wa kidini uwe wa kisiasa hatutaukubali. Hatutaukubali kama Watanzania. Watanzania wanasimama na viongozi wao wa dini kupinga udini, kupinga siasa chafu, kupinga uchonganishi.
Kwa hiyo, tunaungana kwa sauti moja kuiunga mkono serikali yetu ya Daktari Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata yale mambo yaliyotupata 29... tarehe 29 Oktoba mwaka jana, tumeona serikali yetu imeyashughulikia kwa taratibu na kanuni na sheria tulizonazo na yanaendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria zetu.
Kwa hiyo tuache serikali yetu ambayo inaendelea kusimama imara kuona kwamba Tanzania inarudi katika amani yake. Na huu inawezekana ni wivu tu kwa nini tulipita salama tulivuka salama. Eh sasa watuache na nchi yetu ambayo kwa kweli inaendelea kuwa imara na yale ambayo yaliyotufikia au yaliyotupitia yametuiimairisha na yataendelea kutuimarisha zaidi lakini hayatabomoa Tanzania"