Kama kawaida yake uislamu ni dini ya haki na isiyotoa mwanya wa ujanja,utapeli na unyonyaji.
Masheikh mbali mbali wameendelea kuweka wazi msimamo huo wa uislamu ambao umo kwenye Qur'an na suna za mtume Muhammad rehma na amani zimshukie.
Katika ufafanuzi huo,masheikh wamesema kama itatokea muislamu kulazimishwa na mifumo ya kiinchi kuchangia bima kwa lazima basi siku atakapoumwa na ikatibiwa kwa gharama zaidi ya zile anazochangia kwa mwaka basi ni wajibu kwake kuuliza hesabu hizo na tofauti ya juu aliyokuwa hakuchangia basi aitoe sadaka.
Muhimu kuliko yote asitibiwe kwa pesa walizochangia wengine.Atibiwe kwa pesa zake mwenyewe au zilizochangwa na ndugu na wahisanai wake.
View: https://www.youtube.com/watch?v=OjIHAm_536s
Assalaam Alaykum
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote. Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (S.A.W) na Swahaba zake (R.A) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Huyu Bwana kwenye hii clip, ameielewa na kuifafanua Bima (Ta'amyn) kwa mtizamo wa Bima ya maisha. Na huu ni mtizamo tofauti kabisa na Bima ya Afya.
Aidha amefikia hatua ya kuifananisha Bima ya Afya kama ni biashara inayo husisha vitu vitatu ambavyo ni haram navyo ni: Kamari, Riba na
Gharal (biashara isiyo julikana), na hivi vyote havishabihiani (tofauti) kabisa na Bima ya Afya.
Tuanze na ufafanuzi wa
Kamari (Gambling). Kwenye kamari either you gain or you loose hivyo ni mchezo wa kubahatisha (Betting), lakini Binaadamu yeyote duniani (Aliye zaliwa na Mwanamke) katika uhai wake ni lazima ataugua au kushambuliwa na maradhi ( So Maradhi/Uganjwa is a sure to come event) sasa hapo suala la kamari litaingia vipi?
Riba (Interest) Kwa tafsiri ya kawaida ni kwamba Riba ni kitu chochote chenye monetary value, ambacho kinajumuisha fidia, equity, tunu, na hata intellectual property ambayo anapewa mfaidika whether or not the value is readily ascertainable. Sasa hapa kwenye Bima ya Afya mfaidika hapati monetary gain yeyote zaidi ya huduma ya Afya/matibabu anayopewa kwa maana nyingine huyu mfaidika anapata service in kind. Na hata hivyo kwenye makubaliano ya awali na huyo service provider hakuna kipengele cha interest (Riba) yeyote hapo.
Gharal (Kisicho julikana-Intangible). Nadharia hii haihusishi kabisa matibabu yanayo tokana na Bima ya Afya, kwa maana ya kwamba mgonjwa anakwenda Hospitali/Kituo cha Afya/Zahanati physically anatibiwa, kwa kupewa dawa, X-ray, kuchomwa sindano n.k sasa hapo Gharar inaingia vipi?
Sheikh @~Juma kuna mengi ya kujadili hapa, lakini muda ambao si rafiki, itoshe kusema kwenye Bima yeyote imetawaliwa na misingi mikuu mitatu:
1.
Insurable Interest ikiwa na maana ya kwamba wewe mkata Bima una maslahi gani na hiyo Bima?
2.
Indemnity & Subrogation Hii ina maana ya kwamba kiwango cha fidia iwe ya matibabu au chochote ni kile kile ambacho kitakurudisha katika hali ya mwanzo kabla ya kadhia iliyo kupata be it Afya, Kuibiwa etc.
3.
Uberrimae Fidei: Hii ina maana ya kwamba uwe mkweli kwa nafsi yako na kwa Allah (swt), Utmost Good Faith. Na hiki ndio kipengele muhimu ukizingatia imani (Center of contravesial).
Lakini zaidi ya yote ni nani nani kati yetu anaye fahamu kuwa kesho ataugua?
Ni vyema kujiandaa sasa kwa maisha ya kesho
Na tuliyoyateremsha kutoka katika Qur-aan ni uponyaji (moyo) na rehema (ya Mwenyezi Mungu) kwa Waumini
Surah Israh(17)
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atutengenezee mambo yetu na Atuepushe na haramu.