"Ramadhan Cup ni ukosefu wa adabu, ni ukosefu wa adabu, maanake hawa Ramadhan Cup wakitoka kwenye Ramadhan Cup watakwenda Ijumaa Cup, watakwenda masahaba Cup hawa, watakwenda Adhuhuri Cup, watakwenda watakwenda watakwenda mwisho...hebu kuweni na adabu na dini ya Mwenyezimungu. Wote wanayoyafanya hawa nikuambieni Waislamu naomba mnichukie mpaka kiama, yanafanywa haya ni Waislamu watupu, kama nilivyosema kuna wengine huwa hawafungi, wanakula mchana ili usiku waingie wakiwa na afya nzuri, wanakula mchana",- Ujumbe wa Sheikh Hashim Rusaganya ikiwa ni siku chache kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan.