Sheikh Hemed Jalala awatakia Wakristo Heri ya Krismasi

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania, Sheikh Hemed Jalala, amewatakia Watanzania wote, hususan waumini wa dini ya Kikristo, heri ya Sikukuu ya Krismasi inayoadhimishwa duniani kote kama kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wao, Yesu Kristo.

Akizungumza katika salamu zake za sikukuu kwa mwaka 2025, Sheikh Jalala amesema Jumuiya ya Shia Tanzania inatoa mkono wa kheri kwa Wakristo wote kusherehekea siku hiyo muhimu kwa amani, upendo na mshikamano. Ameeleza kuwa Krismasi ni kipindi cha kutafakari thamani ya maisha, kuvumiliana na kuimarisha mahusiano mema kati ya waumini wa dini mbalimbali.

Sheikh Jalala amesema Krismasi ya mwaka huu inakuja katika wakati muhimu kwa taifa, kufuatia matukio ya Oktoba 29 ambayo yaliiacha jamii ikiwa na majeraha ya kijamii na kiakili. Kwa msingi huo, amesisitiza kuwa sikukuu hiyo iwe chachu ya kurejesha amani, umoja na mshikamano ambao kwa muda mrefu umekuwa nguzo ya taifa la Tanzania.

Your browser is not able to display this video.
 
Namkubali sana huyu Sheikh. Ni muislam wa kweli muumin8 mzuri wa kipenzi chetu cha dhati mwamba mkombozi wa waislamu Imam Hussain ibn Ali aliyeuwawa kikatili kuulinda kuutetea na kuupigania uislam dhidi ya dhulma, uonevu ukandamizaji. Kupitia yeye tumepewa tawafiq/tawfeek ( the ability to win and succeed) na tuna uhakika wa jannahlut firdaus.

kwenye picha hapo chini kipenzi chetu cha dhati Imam hussain akimuaga binti yake kipenzi Sakinah kabla ya umauti kwenye battle of Ashura.

 
Hivi hao nao huwa wako Bakwata? Suni ndo bakwata?
 
Hakika huu ndio uislam niujuao na hawa ndio mashehe wa kweli sio wale wakata vichwa.
Mwamba Imam Hussain Ibn Ali kipenzi chetu cha dhati alijitoa nafsi kuupigania, kuutetea na kuulinda uislam dhidi ya dhulma, uonevu na ujandamizaji.

Hapo chini ni battle of Ashura. Farasi Zuljanah kwa nyuma.




adriz de mbusii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…