Sheikh Karume angeshauvunja Muungano

Kwa mawazo haya Zanzibar bado haijakomaa na inabidi tuitawale Hadi watapopata akili ya kujiendesha.

Zanzibar badala ya kuwaza kujitenga na kujiendesha wenyewe bado mnawaza kulelewa na US na Oman (ambao nao ni choka mbaya) na nchi zingine za arabuni. Huu ni uzwazwa

Kwa mawazo hayo Zanzibar mnakuwa kama mtoto ambaye anajiona kakua na kutaka kuondoka nyumbani kwa babaye ilhali bado hajakomaa, baba akiruhusu uondoke wa ajabu atakua ni mzazi na si mtoto, hivyo tutaitawala Zanzibar Hadi tujiridhishe ujinga wa kuwaza kulelewa umewaisha na mpo tayari kujiendesha badala ya kuwaza kubemendwa na USA.
Hivi visiwa vina thamani kubwa sana kuliko madini ya Tanganyika. Akipewa mmarekani ndani ya miaka mitano kutakuwa kama Dubai. Wadangnyika tutakuwa tunazamia kwenda kuomba ajira za kuwafulia nguo na kudeki nyumba za wazanzibari.
 
Hiyo population tu sijui wataiweka wapi.
 
Waache kulalamika. Waje Tanganyika wafaidi flyovers.reli ya kisasa, waoe na kuolewa walime, wachimbe madini. Huku hawataitwa wahamiaji haramu kama wahabeshi! Waje tu ni bure nauli yao tu. Sisi huko tutaenda kama watalii na kununua bidhaa. Kwao tatizo la muungano ni nini.nina jirani mpemba anakaa kwa raha zake. Kubwa tu tunamuita MPEMBA. Hana jina la kutupa sisi atatuitaje wakati kuna mmakonde, mzaramo, mchagga, mhaya .... Kwao tukienda wanasema mbara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sheria za kiislamu, mwanamke hawezi kuvunja ndoa. Tanganyika tutaendelea kuwatawala mpaka tutakapoona faida za kuwatawala ni ndogo kuliko hasara. Ila kwa sasa bado wanatupa raha kuwa nao.
 
Na ndo maana hata Rais wao Wazanzibari anachaguliwa Bara na ni lazima awe chaguo la watawala wa Bara.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.
Naawatakia Muungano mwema huku nikisisitiza
Nautakia huu muungano wetu adhimu udumu milele na hivyo kukitokea yoyote anayetaka kuuchokoa muungano, namshauri chokochoko amchokoe pweza, muungano hutauweza kwasababu tutaulinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia muungano mwema.
P
 
Mm huwa nachukizwa pale mtu anavyozungumzia vibaya muungano wetu adhimu hivi mmekosa vya kuzungumza
 
Alichokipanga Mwl. Nyerere kukipangua ni mpaka sijui uwe na akili ya namna gani! Angalia suala la azimio la Arusha mpaka leo tunatamani lirudishwe. MPAKA KESHO IMANI YANGU NYERERE NI NABII.
Pamoja na mazuri yake mengi kwenye huu Muungano alifeli na ndio maana mpaka leo unadumu kwa nguvu za kijeshi. Aidha hata Azimio la Arusha tija yake ilikuwa ya kinadharia zaidi kuliko kiuhalisia.
Tunachojisahaulisha ni kwamba HAYATI BABA WA TAIFA ALING'ATUKA BAADA YA UCHUMI NA VIWANDA KUWA VYOTE VIMEKUFA.
HAKUWA NABII WALA MUNGU NA NDIO MAANA KWA UUNGWANA ALIOKIWA NAO ALIKIRI KUFELI NA AKAACHA ANDIKO "TUJISAHIHISHE!"
 
Alichokipanga Mwl. Nyerere kukipangua ni mpaka sijui uwe na akili ya namna gani! Angalia suala la azimio la Arusha mpaka leo tunatamani lirudishwe. MPAKA KESHO IMANI YANGU NYERERE NI NABII.


Yaani Laanatullahi Nyerere ni Nabii wako wa ufisadi na wizi??

Hivi upiganie kununua shamba au kujenga nyumba yako , unajinyima kula na kuvaa , mwisho wa siku anakuja Laanatullahi wako Nyerere anakuambia tunaichukua hii nyumba , Jambazi hilo unalita Nabii ??

Lazima utakuwa ni mwanachama kwenye hiyo biashara yake
 
Karume alikuwa ni mtu anayehitaji muungano kuliko mtu yoyote kwa staili ya uongozi wake wa mabavu asingekuwa salama umma party walikuwa wanamsumbua sana na hakuwa na nguvu kuwazuia zaidi ya kutegemea bara
 
Poke sana kwa mawazo yako yasiyo tanuka.


MAGUFULI4LIFE.
 
Mtakatifu Nyerere.


MAGUFULI4LIFE.
 
Mapinduzi Mapinduzi Daima...
 
Watanganyika wamejaa tele kitope, chujwani kiboje na kwengineko, ujidanganye tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…