Sol de Mayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 6,515
- 6,230
Bilionea kutoka familia ya Kifalme Abu Dhabi, Sheikh Khaled Bin Zaed Al Nahyaan yuko katika hatua ya mwisho kuinunua New Castle United kwa kitita cha pauni Milioni 350.
Sheikh Khaled yupo katika mazungumzo ya mwisho na Mike Ashley ambae ni mmiliki wa klabu hiyo
Sheikh Khaled ni binamu wa Sheikh Mansour ambae ni mmiliki wa Manchester City.
Waarabu sio watu wa spotispoti jamani 😁😁 Mungu amewabariki sana hawa ndugu zetu, sipati picha hawa mabeberu wa kizungu wakiona matajiri wa kiarabu wakimiliki klabu ndani ya nchi zao, Mfano PSG, Man City, kama sikosei na West Ham na sasahivi wako katika hatua ya mwisho kuinunua New Castle.