Sheikh Kishki: Tuna bahati sana ya kuwa na Mufti anayekubalika kitaifa na kimataifa

Sheikh Kishki: Tuna bahati sana ya kuwa na Mufti anayekubalika kitaifa na kimataifa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
"Sisi waislamu wa Tanzania tunashukuru sana Allah kwa sababu sasa mufti tuliyenaye anakubalika sana. Taasisi za kitaifa na kimataifa na serikali za nchi mbalimbali duniani kote huko Mufti wetu anakubalika sana..."TUNA BAHATI YA KUWA NA MUFTI ANAYEKUBALIKA"

"Awali tulishuhudia mashindano makubwa ya kimataifa yaliyoshirikisha nchi zaidi ya thelathini hapa Tanzania. ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania na sasa unasimamia mashindano makubwa ya kwanza ya kimataifa ya wasichana ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza na kwa namna unavyokubalika nchi kumi na moja zilizofuzu zinakuja Tanzania chini ya usimamizi wako. Mashindano ya aina hii na kwa ukubwa huu hayajawahi kufanyika kote duniani. Allah Akupe umri mrefu"

Sheikh Kishki aliyasema hayo jana Ijumaa 9.8.2024 kwenye ukumbi wa mfalme Mohammed VI kwenye kikao cha kamati ya maandalizi ya mashindano ya dunia ya wasichana ya Qur ani tukufu.

Kikao hicho cha kamati ya maandalizi kiliongozwa na Samaha Mufti wa Tanzania Dr. Abubakar Zubeir Ali Mbwana.

🔷 Mashindano hayo yanayoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania yatafanyika tarehe 31.8.2024 kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

🔷 Mgeni rasmi kwenye Mashindano hayo ni Rais wa Tanzania Dr. Samia Suluhu
.....

Dr. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa Mufti
Mwenyekiti kamati ya habari na uhamasishaji
Jumamosi 10.8.2024
Dar es salaam
 
Back
Top Bottom