Sheikh Kwezi: Tusiwakosoe viongozi wakuu hadhari kwa kisingizio cha Demokrasia

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wito umetolewa kwa Watanzania kuendeleza desturi ya muda mrefu ya kuwaheshimu viongozi na kwamba hata pale inapoonekana kuna ulazima wa kuwakosoa, basi ukosoaji huo utanguliwe na staha ya kuwaheshimu viongozi wahusika

Wito huo umetolewa leo, Jumamosi Juni 07.2025 na Sheikh wa mkoa wa Simiyu Sheikh Issa Kwezi wakati akitoa Mawaidha baada ya kujumuika pamoja na Waislamu wengine kwenye Swala ya Eid Adh-ha mkoani humo

"Watanzania mara zote tumesimama katika maadili ya kuheshiana, mdogo anamuheshimu mkubwa na yule asiyekuwa na cheo ambapo yeye anaongozwa anamuheshimu yule ambaye anamuongoza, na hizo ndio tamaduni zetu, lakini leo tunaona mpaka watu wazima wamepoteza maadili kwa kisingizio tu cha demokrasia" -Sheikh Kwezi

Your browser is not able to display this video.
 
 

..wanaharakati kulawitiwa wanapokamatwa ni ukosefu wa maadili Shekhe alipaswa kuukemea.
 
ni kwa sababu viongozi waliopo ni waislam wenzie, ila wangekuwa wa dini ingine angeongea vingine. shehe hajawahi kutekwa wala kupotelewa na ndugu, ndio maana hana uchungu na haelewi uhalisia wa uchungu wake upoje. shehe angekuwa babake SATIVA aliyetupwa aliwe na fisi angeongea hayo? shehe angekuwa babake mdude, babake soka au babake shehe aliyeokotwa kafa zanzibar, angejua uchungu na kutoa ushauri bora kwa viongozi. kama hawasikii sirini lazima lisemwe hadharani.
 
Shehe ubwabwa huyo, katupia kanzu ya chama cha mbogamboga!

Shehe anayejitambua na asiye mnafki ni Shehe Ponda.
Anahubiri kwa uwazi neno HAKI!
 
Kwa nini usiwaambie na viongozi waendeleze desturi ya kuthamini haki ya kuishi, haki ya kuchagua na kuchaguliwa n.k
 
No reform no election
 
Lengo la upinzani kuwepo ni kwa ajiri ya kukosoa mabaya yanayofanywa na serikali
Huyu anaezuia serikali kukosolewa ana uelewa wowote kuhusu utawala?
 
Usha wahi kuona mvaa kobazi anaakili?
 

NRNE
Usha wahi kuona mvaa kobazi anaakili?
NRNE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…