Sheikh Mohamed Nassor na Kibao cha Mtaa wa Sheikh Badi Lindi

Sheikh Mohamed Nassor na Kibao cha Mtaa wa Sheikh Badi Lindi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SHEIKH MOHAMED NASSOR NA KIBAO CHA MTAA WA SHEIKH MUHAMMAD YUSUF BADI

Mashaallah Sheikh Muhammad Nassor kasimama chini ya kibao cha Sheikh Muhammad Yusuf Badi kilichopo mjini Lindi.

Sheikh Mohamed Nassor alikuwa Lindi kuhudhuria mazishi ya Sheikh Badi.

Sheikh Badi ndiyo mwalimu aliwasomesha Rashid Salum Mpunga na Yusuf Mohamed Chembera katika madrsa yake walipokuwa watoto wadogo.

Wanafunzi hawa wawili waasisi wa TANU ndiyo waliomtia mwalimu wao ndani ya TANU mwaka wa 1956.

1668719838539.png



TANU ilipata nguvu kubwa Sheikh Badi alipojiunga na TANU.

Julius Nyerere alipokwenda Lindi kwa mara ya pili mwaka 1956 (safari ya kwanza ilikuwa 1955) Mwalimu alipokelewa kwa zafa na wanafunzi wa madrasa ya Sheikh Muhammad Yusuf Badi.

Siku ya uhuru wa Tanganyika 9 Sesemba 1961 hotuba ya kupokea uhuru ilisomwa na Yusuf Mohamed Chambera na hotuba iliandikwa na Sheikh Muhammad Yusuf Badi.

Hotuba yenyewe ilikuwa Kunut dua inayosomwa kila Sala ya Alfajir.
 
Kumbe lindi ina barabara nzuri na taa za sola?
 
Back
Top Bottom