Sheikh Suleima Mohammed Ulatule (99), amezikwa katika makaburi ya Nyang’andu kivule jijini Dar

Sheikh Suleima Mohammed Ulatule (99), amezikwa katika makaburi ya Nyang’andu kivule jijini Dar

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Shura ya Maimamu Tanzania

MAZISHI YA SHEIKH MWENYE UMRI MKUBWA ALIYEFIA GEREZANI

Sheikh Suleima Mohammed Ulatule (99), amezikwa jana tarehe 20/12/2024, saa 11:00, jioni katika makaburi ya Nyang’andu kivule frema kumi jijini Dar es Salaam.

Sheikh Ulatule alikua gerezani kwa miaka 9, akituhumiwa na serikali kwa kuvamia kituo cha polisi cha stakishari jijini Dar es Salaam toka mwaka 2015. Tofauti na masheikh wengine waliohusishwa naye katika tuhuma hizo, yeye alikamatwa na familia yake ya watu 15.

Baada ya masiku kadhaa ya kutofahamika walipopelekwa, hatimaye (yeye na watu wake 7), walikutwa katika gereza la segerea jijini Dar es Salaam baada ya kufikishwa Mahakamani na kusomewa shtaka hilo (Watu wake 9, wengine waliokamatwa pamoja naye hawajulikani walipo mpaka leo).

Akiwa mikononi mwa watu wa usalama (kabla ya kupelekwa Mahakamani), Sheikh Suleiman na wenzake waliteswa sana, hali ambayo ilipelekea ugonjwa katika maisha yake yote ya gerezani.

Katika hali hiyo ya kuathirika kiafya, tarehe 9/12/2024, alizidiwa akapelekwa hospitali ya Amana Ilala ambako alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Baada yakupata nafuu iliyomuwezesha kunywa uji alitolewa (ICU), tarehe 12/12/2024, na kurejeshwa gerezani. Akiwa taabani gerezani tarehe 16/12/2024, alizidiwa na Mkuu wa Gereza aliamuru arejeshwe tena hospitali ambako alifikishiwa tena (ICU).

Tarehe 19/12/2024, hali ilizidi kuwa mbaya na ilipowadia saa 8:00, adhuhri Sheikh Suleiman Ulatule (99), alifariki dunia. Siku hiyo hiyo viongozi wa Shura ya Maimamu Tanzania walikwenda hospitali na kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Tarehe 20/12/2024, viongozi wa Shura ya Maimamu wakiambatana na watu wa familia yake walikwenda gereza Kuu Ukonga kwaajili ya kufuatilia taratibu za kupata mwili wa marehemu.

Uongozi wa gereza ulikamilisha taratibu zake za kisheria ikiwa ni pamoja na kumtoa afisa wa jeshi hilo kuungana na ndugu wa marehemu kwaajili ya kufanikisha hatua nyingine za kisheria.

Upande wa familia na Afisa wa Magereza walikwenda kukutana na uongozi wa Jeshi la Polisi ambalo na wao pia walikamilisha taratibu zao za kisheria zilizowawezesha Shura ya Maimamu na familia kwenda hospitali ya Amana ulipo mwili wa marehemu kukamilisha hatua muhimu za kukabidhiwa mwili.

Shura ya Maimamu ilitoa taarifa na kuandaa mazishi ya marehemu. Aidha kutokana na mwili kupatikana muda wa nusu ya siku (saa 7:30, adhuhuri), na taarifa ya mazishi kuwa ya muda mfupi, na pia mahala pa mazishi kuwa mbali, watu wengi hawakupata fursa ya kuwahi mazishi.

Shura ya Maimamau inawashukuru wale wote waliotoa mchango wa hali na mali katika mazishi hayo.

Aidha ifahamike kabla ya kifo hiki, kilitanguliwa na kifo cha mdogo wake Sheikh Suleman Mohammed Ulatule, Saidi Mohammed Ulatule (79), ambaye naye kama kaka yake alifia gerezani mwaka uliopita 2023. Kwa vifo hivi viwili, wanafamilia waliobaki mahabusu ni:

1. Ali Mohammed Ulatule (70).
2. Khamisi Mohammed Ulatule (61).
3. Nassoro Suleiman Ulatule (41),
4. Rajab Ali Mohammed Ulatule (34).
5. Ramadhani Khamisi Mohammed Ulatule (29).

Aidha jumla ya Masheikh wanao endelea kusota gerezania kwa zaidi ya miaka 9, sasa ni 51, (wakiwemo hao wa familia ya Ulatule). Shura ya Maimamu Tanzania inawakumbusha watanzania wote kuwasaidia watu wenye kustahiki msaada na kutetea haki za binadamu bila ya kujali rangi, kabila, dini, siasa wala taifa.
Tunatumia tena fursa hii kuwashukuru wale wote waliotoa mchango wa hali na mali katika mazishi haya ya Sheikh Suleiman Ulatule.
IMG-20241221-WA0018.jpg
IMG-20241221-WA0019.jpg
IMG-20241221-WA0020.jpg
IMG-20241221-WA0021.jpg
IMG-20241221-WA0022.jpg
IMG-20241221-WA0023.jpg
 
Ilikuwaje wakamng’ang’ania mzee wa miaka tisiini?

Ok mwanzo sikusoma arifa yote,lakini kwanini familia ya Ulatule ina mahabusu wengi sana tena wa ubini mmoja?yaani hakuna mjomba au mtu kutoka nje ya kiuno cha Ulatule kuna shida gani?labda ndiyo waliotoa eneo kituo kijengwe wakaanza harakati za kutaka baadhi ya ardhi yao irudi wakapewa kesi?

Mungu amrehemu.
 
Samahani waheshimiwa, hivi hii familia ilikamatwa mwezi wa ngapi huo mwaka wa 2015 kwa hizo tuhuma za ugaidi? Na hao watu 9 waliokamatwa nao walikuwa ni akina nani, na wana asili ya wapi? Na kwa nini mpaka muda huu hawajulikani walipo?

Chanzo hasa hasa cha kukamatwa kwao kilikuwa ni ugaidi wa nini? Na kwa nini DPP ameona hana sababu tena ya kuendelea na hiyo kesi baada ya miaka 10 kupita? Je, watalipwa fidia kwa mateso yote waliyopitia kwa kukaa mahabusu miaka 10?

Maana ukirejea kwenye kumbukumbu, 2015 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi na hivyo Rais wa wakati huo alikuwa ni JK. Kuanzia Novemba, 2015 ndiyo JPM alichukua madaraka.
 
Hatimae ndugu wa uteule wametoka gerezani tarehe 3.3.2025
Wale walotoka wamekamatwa tena wote na kirudishwa Gerezani. Umefurahia uraiani masaa machache sana. Wenzao wakitoka mahakamani wanakimbia.. Wao wakaitwa Stakishari wakaenda. Ndo hawajarudi tena
 
Back
Top Bottom