Sheikh Suleiman Takadir alivyopotea katika historia ya Uhuru wa Tanganyika

Sheikh Suleiman Takadir alivyopotea katika historia ya Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUTOKA FB: SHEIKH SULEIMAN TAKADIR ALIVYOPOTEA KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said July 11, 2017 0

Mohamed Said Salum
Ugomvi kati ya Sheikh Suleiman Takadir na Mwalimu Nyerere ndani ya ofisi ya TANU pale New Street ni katika matokeo ya historia ya TANU ambayo wana TANU wenyewe walipenda labda yafutike yasijulikane.

Nadhani hata Mwalimu Nyerere hakupenda ugomvi ule uingie katika historia yake.

1574674341709.png

Sheikh Haidar Mwinyimvua

Hakika ni kisa cha kusikitisha. Ugomvi huu alinihadithia marehemu Mzee Haidar Mwinyimvua baba yake Sheikh Ahmed Haidar ambae alikuwapo katika mkutano ule 1958 mara tu baada ya TANU kuamua kuingia katika Kura Tatu.

Dr. Tamim ndiye aliyenipeleka kwa Mzee Haidar nyumbani kwake Magomeni. Alinieleza historia nzima ya Sheikh Takadir na ya Nyerere katika siku zile za mwanzo hadi Sheikh Takadir alipofukuzwa TANU.

Kisa kizima nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

scan0026.jpg

Kushoto ni Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia na Julius Nyerere

Mohamed Said Salum Wakati wa utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes sikuweza kupata picha ya Sheikh Takadir popote ikawa kama vile huyu mtu hakuwa katika TANU tena kiongozi wa juu kabisa.

Picha yake ya kwanza nilikuja kuipata miaka hii ya 2000 na alinipa rafiki yangu marehemu Abdallah Kihombo nyumbani kwake Ilala.

Baadae nikapata nyingine kutoka kwa Jim Bailey African Archive, Johannesburg...

DSCN0101.JPG

Kushoto Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadiri, Clement Mtamila na Titi Mohamed
Nyuma ya Nyerere, Mama Maria Nyerere, Rajab Diwani na John Rupia
 
Tunashukuru sasa amepatikana. Umefanya kazi njema sana. Miaka mingi hakuwa akionekana.sasa tunamwona.
 
Ungetwambia kabisa sababu ya ugomvi wake na Nyerere ulikua upi; isije ikawa mambo ya Lipumba leo. Mtu yupo upinzani kumbe anacho kifanya USIKU anakijua mwenyewe, so sema what was the reason of their conflict
 
Huo ugomvi ulikuwa unahusu nini na Chanzo chake kilikuwa ni kipi, na kuna madhara gani yaliyotokana na Ugomvi huo?

Romaxtim
 
Mtoa uzi umeanza vizuri then umenichanganya mbona huelezei ugomvi huo wakati wewe ulihadithiwa?,picha zako nimezipenda sasa zingeendana na mchango wako makini ingekuwa vema sana,ila kwa jinsi hii inaonekana kama mazungumzo ya kijiweni.
 
Mkubwa wangu Mo'd said umeniacha njia panda nilitarajia utaeleza kisa cha mzee Takadiri kupotea katika siasa za tz lakini inaonekana kana kwamba kitabu hakinunuliwi hivyo unakitangaza kiaina,lkn ungekieleza kisa hiki lau kwa ufupi hamu ya kupata kitabu kizima ingekuwa imeongezeka.
 
Back
Top Bottom