Sheikh Suleiman Takadir na Agenda ya Waislam katika Tanganyika huru 1958

Sheikh Suleiman Takadir na Agenda ya Waislam katika Tanganyika huru 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
TUJIKUMBUSHE FIKRA ZA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NA MSIMAMO WA TANU WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

Mwaka wa 1958 TANU ilikuwa imevuka kiunzi cha Kura Tatu kilichotaka kukigawa chama katika mapande mawili na pengine moja lingetoka na kuanzisha chama kipya.

TANU ilibaki moja lakini wako waliojitoa na kuanzisha vyama vipya - Zuberi Mtemvu alijitoa na kuunda Congress na Mashado Ramadhani Plantan na kikundi kidogo wakaunda AMNUT.

AMNUT iliundwa kwa kusudio la kulinda maslahi ya Waislam katika Tanganyika huru.

Kura Tatu iliwaondoa Waislam katika ulingo wa siasa na kuleta watu waliokuwa nje kabisa ya kupigania uhuru ingawa na wao waliutaka uhuru lakini walikuwa pembeni kwa sababu hii na ile.

Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza hali iliyomkabili Mwalimu Nyerere ndani ya TANU akiwa kazungukwa na Waislam katika harakati za kupigania uhuru.

Tujikumbushe joto na upepo ule mkali uliokuwa unavuma pale ofisi ya TANU New Street na Tanganyika nzima:

''Nyerere alikubali ukweli kuwa kulikuwa na upogo baina ya Waislam na Wakristo hususan katika elimu ambayo itawazuia Waislam kushika nafasi za uongozi katika serikali ya wananchi.

Nyerere aliwaomba Waislam waweke matumaini yao kwa TANU ambayo itaanzisha mabadiliko ya lazima kuwainua Waislam kwenye nafasi za usawa pamoja na Wakristo mara tu uhuru utakapopatikana.

Lakini hili, Nyerere aliwakumbusha Waislam mara kwa mara kuwa linaweza kufanyika tu kwenye Tanganyika huru na siyo chini ya utawala wa Kiingereza.

Waislam katika TANU, kwa upande wao, waliamini kwamba ilikuwa kinyume kwao kuanzisha chama cha kisiasa chini ya maslahi ya kikundi kimoja kama ndiyo lengo la kudai uhuru.

Hili, wengi waliamini, lingesaidia kuunda vikundi vingi na kusababisha mfarakano.

Kwa kweli madai yaliyokuwa yakitolewa na AMNUT hayakuwa madai ambayo yangetolewa kwa TANU katika wakati ule.

Vita vya mwaka 1947 kati ya India na Pakistan vilivyosababisha kupoteza maisha ya watu wengi, vilikuwa bado vinakumbukwa na watu wengi.

Chanzo cha ugomvi huo kilikuwa ushindani baina ya Waislam na Wahindu.

Kabla ya mwaka 1947 India na Pakistan zilikuwa nchi moja chini ya ukoloni wa Mwingereza.

Waislam na Wahindu walipigania uhuru pamoja na walifarakana mara tu ilipokuwa wazi kuwa Uingereza ingetoa uhuru kwa India.

Watu wengi nchini Tanganyika walihofia kwamba kuruhusu fikra kama zile zilizotolewa na Sheikh Takadir kuota mizizi kulikuwa kukaribisha ile hali ya India na Pakistan Tanganyika.

Nyerere alionya kuwa hakutaka hali kama ile ije kuisibu Tanganyika."

Picha: Kulia wa kwanza ni Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na kushoto ni John Rupia amemziba Julius Nyerere Katikati aliyeshika tama ni Zubeir Mtemvu.

Picha hii imepigwa kwenye tawi la TANU alilofungua Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa mwaka wa 1954.
 
Angalia picha:

Screenshot_20201206-042737.jpg
Screenshot_20201206-042913.jpg
Screenshot_20201206-043036.jpg
 
Asalam aleiku ndugu mohamed said. Una maoni gani kuhusu 20 kwa 3? Na ni nani wa kulaumiwa?
 
asalam aleiku ndugu mohamed said. una maoni gani kuhusu 20 kwa 3? na ninani wa kulaumiwa?
Madax...

Jibu langu unalo wewe sasa nitakuuliza tupate jibu la swali lako.

Hebu fikiria Rais Muislam kaunda Baraza la Mawaziri kachagua Waislam 20 na Wakristo 3.

Unadhani hali ingekuwaje?
 
Madax...

Jibu langu unalo wewe sasa nitakuuliza tupate jibu la swali lako.

Hebu fikiria Rais Muislam kaunda Baraza la Mawaziri kachagua Waislam 20 na Wakristo 3.

Unadhani hali ingekuwaje?
2025. Rais atakuwa muislamu.
Ningependa baraza lake liwe na waislamu tupu,manaibu waislamu tupu.
Sina uhakika kama nitapungukukiwa na kitu
 
Madax...

Jibu langu unalo wewe sasa nitakuuliza tupate jibu la swali lako.

Hebu fikiria Rais Muislam kaunda Baraza la Mawaziri kachagua Waislam 20 na Wakristo 3.

Unadhani hali ingekuwaje?
kwangu mie hata wakijichagua mashehe watupu maadam hawazui kula yangu, uhuru wangu watajua wao wenyewe
 
Back
Top Bottom