Sheikh Ramadhan Twawilu ametoa wito kwa viongozi wa dini kutumia nyumba za ibada kukemea wote wenye mipango ya kufanya vurugu na kuhatarisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi akisisitiza kuwa watu hao ni waumini ambao wapo katika nyumba hizo za ibada.
Sheikh Twawilu ambaye ni Katibu wa Kadhi(BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, ameyasema hayo akiwasilisha mada katika Kongamano la Amani Kanda ya Magharibi lililofanyika mkoani Tabora leo Oktoba 24, 2025
"kuna baadhi ya watu ambao hawakitakii mema Taifa letu la Tanzania kuonyesha ishara ya kutaka vurugu itokee sisi kama viongozi wa dini hatuwezi tukalifumbia macho jambo hilo maana hawa wanaotoa viashiria hivyo ni waumini wetu kama haingii msikitini anaingia kanisani ni lazima tukemee jambo hilo"