SI KWELI Sheikh Yahya Hussein alitabiri baada ya Rais Mwanamke kumaliza Mihula yake Upinzani utaongoza nchi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Na huyo Sheikh yahya alikuwa mtaalamu sana wa hesabu za nyota katika kutabiri. !

Ngoja tusubiri tuone. !
 
Kuna kitu nimeona mtandaoni kina trend sana kwamba Sheikh Yahya alisema baada ya Rais mwanamke upinzani utachukua nchi. Binafsi nimefurahi sana maana mtabiri huyu nilikuwa namkubali sana.

 
Asanteni sana JamiiCheck kwa ufafanuzi huu. Tumedanganywa sana kumbe hakuwahi kusema, RIP Sheikh Yahya
 
Kumbe hakusema, watu wanajua kudanganya aisee. All in all, upinzani komaeni, maneno haya yanaweza kutumia
 
Nakumbuka alisema Rais atakuwa mwanamke au upinzani utashinda

Pia alitabiri tarehe ya mwisho wa Dunia. Kilichotokea kwenye tarehe ile aliyoitaja Hakukuwa na mwisho wa Dunia ila kwenye tarehe ile yeye mwenyewe alifariki.
 
Sasa kama kweli amesema hayo, mnawezaje kusema "Si kweli"??? Mmeniangusha jamiicheck mmekua Jamii heck
 
Upinzani gani unaozungumzia au huu upinzani unaompa tuzo samia
 
Kwenye miaka ya Sabini huyu mzee alikwenda Tanga kutabiri, watu wanaingia mmoja mmoja anamtabiria, akaingia mama yangu mmoja hivi akamwangalia akampa pole akamwambia "huna raha kwa vile hujajaaliwa mtoto pole sana", kiuhalisia yule mama alikuwa na watoto 12 hadi mapacha mara mbili kuanzia hapo hakutaka tena upuuzi wa kutabiriwa, binafsi tangu aliponisimulia hiyo habari sikupenda kusikiliza au kusoma utabiri wake.
 
Na huyo Sheikh yahya alikuwa mtaalamu sana wa hesabu za nyota katika kutabiri. !

Ngoja tusubiri tuone. !
ALICHOTABIRI SHEKHE YAHYA SI HIKI MNACHOANDIKA ULIZENI MJUE,NA KATIKA HUO UTABIRI MAWILI YAMETOKEA TUNASUBIRI LA TATU NA NNE
KWANI ALITABIRI VITU 4
 
πŸ˜€πŸ˜€ Au alichanganya mafile kidogo
 
JamiiCheck nendeni channel 10 mkaombe tape zao za kipindi cha Sheikh Yahya ndio mtapata hayo majibu na sio kumhoji Mtangazaji ambae kumbukumbu zake ndio imekua chanzo chenu kusema SI KWELI. Mngewahoji hata hao waandishi wengine. Sema huyo mtangazaji Elvan Stambuli mliyemhoji kavu kweli, yaani Rais JPM anamuita 'huyo bwana'πŸ˜„πŸ˜„
 
Uliyeweka uzi uliomesha nukuu ya utabiri wa Sheikh Yahya, umesahau kitu kimoja katika kuongeza maneno yako. Hapo kwenye screenshot baada ya neno mwanamke kuna alama (") hii inamaanisha ndiyo mwisho wa nukuu ya maneno yake.


Hayo mengine mmeongeza wenyewe bila kuiona funga semi. Tunajua mnq ndoto upinzani uchukue nchi na hapa mnatengeneza mazingira mkishindwa mliibiwa kura maono ya Sheikh yameonesha mnashinda.
 
Binafsi nilitazama hiko kipindi na.nathibitisha alitabiri upinzani kushinda nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…