Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,962
- 721
Kuna vitu vingine vinahusu tamaduni ya sehem husika. Hiyo ndiyo zanzibar wao wamejitahidi saana kuwa wanavyoona inafaa kwao kuliko kuiga.Nilijaribu kuangalia hii picha kwa makini sikuweza kupata jibu mapema. Nilifikiri jamaa yuko msikitini lakini hapa anasaini fomu za kugomea Urais Zenji mbele ya Jaji mkuu wa Zanzibar (Mh. Hamid Mahamoud). Angalia picha sehemu yenye mzunguko mwekundu.
Mwenye maoni tofauti....
Kuna vitu vingine vinahusu tamaduni ya sehem husika. Hiyo ndiyo zanzibar wao wamejitahidi saana kuwa wanavyoona inafaa kwao kuliko kuiga.
Hebu angalia hapo pahala panafanana na kitu ofisi?Mh... Zanzibar wanakaa ofisi pekupeku kama bata?
Nilijaribu kuangalia hii picha kwa makini sikuweza kupata jibu mapema. Nilifikiri jamaa yuko msikitini lakini hapa anasaini fomu za kugomea Urais Zenji mbele ya Jaji mkuu wa Zanzibar (Mh. Hamid Mahamoud). Angalia picha sehemu yenye mzunguko mwekundu.
Mwenye maoni tofauti....
Hebu angalia hapo pahala panafanana na kitu ofisi?
Hiyo picha ukiangalia utakuta Jaji Mkuu Hamid Mahmoud (Kati kati) na Jaji wa Mahakama Kuu Mh. Mshibe Ali Bakar (kushoto) wote wamevua viatu, ikiashiria kuwa eneo walipo ni safi na haliruhusiwi kuingia na viatu kwa mtu yeyote.
Dr. Shein alikuwa nyumbani kwake na hao jamaa walienda kumfuata ili kumsainisha fomu zake?
Bila ya shaka.
Mkuu wewe ni mwenyeji huko Zenji, naomba niambie kuna ofisi yoyote ya serikali (SMZ) au taasisi ya umma ama idara/kitengo cha SMZ ambayo watu wakiwa ofisini wanatakiwa kuvua viatu?
Ni kweli zipo ofisi za umma Zanzibar ambazo kuna maeneo maalum, kwa sababu maalum, watu hawaruhusiwi kuingia na viatu.
Hapo bila shaka ni nyumbani siyo ofisini. Kwani kuna tatizo gani? Huyo bwana ameishaanza kupewa heshima ya Urais hata kabla ya kupigiwa kura. Ni ishara ya awali kwa mavu (Maalim) kuwa hana lake kwenye urais. Kwa hiyo ajitayarishe kwa nafasi mojawapo ya umakamu...hata mimi naanza kuwa na wasiwasi kwamba hapo ni nyumbani kwa Dr.Shein.