Uliona hata Speaker Sitta alivyouongoza mjadala huu? Tuachane na mawazo finyu kwamba kuna badiliko lolote la maana linaweza kuletwa na Bunge letu hasa baada ya vikao vya NEC ya CCM kutoa angalizo kwa Sitta.
Mimi huwa naota siku ambayo wananchi watapunguza ushindi wa CCM katika Bunge na Serikali za mitaa ANGALAU kwa robo tu ndipo nikubali kwamba sasa wa-Tanzania wanahitaji mabadiliko - wanatuma ujumbe maalumu kwa viongozi. Lakini kila uchaguzi ni ushindi wa kishindo! Hapo tena mbunge gani awe na ujasiri wa kupingana na Chama kikiamua kushikilia msimamo wake?
Wapiganaji wa ufisadi CCM wanapigania nini? Sishangai unafiki ulioonyeshwa na shelukindo/mwakyembe/sitta/manyenye/sendeka/kilimba/mpendazoe katika kuhitimisha suala la RICHMOND..
Nasikitika sehemu kubwa ya jamii bado haijawaelewaa vemaa wanafiki hawa wa demokrasia nchini. kwa hili natumai adhabu yao INAKUJAAA...
Chama ni watu na hakuna kama hakuna watu. Hivyo kama watu ni wanafiki basi chama ndicho kinafiki. Huwezi kutenganisha kichwa na kiwiliwili bado ukawa na mtu kamili!!!!! Huwezi kutenganisha chama na wanachama wake halafu bado kikawa chama!!!!Watu pipoooooooo. CCM si wanafiki ila watu ndio wanafiki kwani unakumbuka ya Dr. H. Mwakyembe? ni CCM hiyo lakini unajua unafiki upo kwa hao Mafisadi si CCM. CCM safi Kikwete safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii spika safi?
Hofu ya uchaguzi imetanda....Hivi kuna mtu ameona 'Speed and standards" katika Bunge hili? Mie sijaona labda nyie wenzangu.....
Dr. Mwakyembe na Selelii wamesema nini kwenye huo mjadala hapo jana?
Ukimwondoa Dr. Slaa na Christopher ole Sendeka, wabunge waliobaki kwenye vita ya Ufisadi waliobaki ni wasanii.
Ukimwondoa Dr. Slaa na Christopher ole Sendeka, wabunge waliobaki kwenye vita ya Ufisadi waliobaki ni wasanii.
I beg to differ! Ole Sendeka ni type ya wale watu wanaouma na kupuliza he is not fit to be called 'mpiganaji wa kweli'!
.Mwakyembe na Selelii wote wamekalia makuti makavu majimboni watokako pamoja na Mpendazoe, kwahiyo ndio maana wamekubali yaishe pengine mafisadi watawaonea huruma warudi mjengoni!! Kulikuwa hakuna sababu ya kusalimu amri dakika za mwisho kama ni kuogopa kuenguliwa na ccm wakati wa uchaguzi, kuna falling back position ya kuwa Independent; hawana sababu ya msingi ya kuthrow in the towel!!
Sure, huyu ni Kamanda mkweli na hafichi chochote! mean slaa Dr
.Maelezo haya hapa chini yanayohusu Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imenisikitisha sana kwa jinsi Kamati hiyo ilivyotishiwa nyau na mambo ya "Posho Mbili kwa kazi moja!"
Source: Mwananchi
Mimi sioni, kwa kauli za Shellukindo kama tuna wapambanaji katika vita hii ya ufisadi! Mjadala wa Richmond ndio huo umezikwa rasmi jana, wapambanaji (ukimwondoa Dk Wilbrod Slaa na Christopher ole Sendeka) wanaonekana walinywea kama wamenyeshewa mvua maskini! Hata hivyo nimefurahishwa sana na jinsi Dk Wilbrod Slaa alivyopambana mpaka mwisho! Soma kauli yake hapa chini:
SOURCE: Mwananchi
Hongera sana Dk Wilbrod Slaa! Upambanaji wako utakumbukwa daima na Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu!
.
Tangu mwanzo tulisema wapiganaji ndani ya ccm,wanapigania matumbo yao na ya watoto wao,lakini baado wenye mawazo finyu wakasema wanapigania maslahi ya taifa.Hayo ndiyo masalahi ya taifa?